X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

  - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 19/Jul 12:20

BODI YA NEEC YATEMBELEA WANUFAIKA WA SANVIN

NA EMMANUEL MBATILO, PWANIMWENYEKITI wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Profesa Aurelia Kamuzora amesema kutokana na uhitaji mkubwa na uwezo wa kurudisha mikopo kwa wanufaika wa mikopo inayotolewa kupitia mradi wa SANVIN Viwanda, wameona kuna haja ya kupandisha kiwango cha mikopo kutoka Milioni 500 hadi kufikia Bilioni moja.Ameyasema hayo Julai 18,2025 Mkuranga mkoani Pwani,katika kiwanda cha Amiron Medical Equipment Ltd, akiwa na wajumbe wa bodi hiyo katika hitimisho la ziara yao ya kutembelea wanufaika wa mradi huo ambayo iliyoanza Julai 15 2025 katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.Prof. Kamuzora katika ziara hiyo akiwa na wajumbe wa bodi,ameonesha kufurahishwa na kuridhishwa utendaji wa mnufaika wa mradi wa SANVIN Viwanda,(Scheme) katika kiwanda cha uzalishaji wa vifaa tiba cha Amiron Medical Equipment ambapo amesema kuwa uwekezaji huo ni chachu ya mageuzi ya kiuchumi kwani itaongeza fursa ya ajira kwa vijana."Ni kitu kikubwa kimefanywa na SANVIN tunaona watanzania wenzetu wenye maono mazuri na ametueleza vizuri jinsi gani ambavyo amejipanga kuuza nje katika nchi za SADC" Profesa Kamuzora amesema.Wakati huo huo,Profesa Kamuzora akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa bodi hiyo amesema wameameahidi kuwaita wadau wote wa mradi huo kuona namna bora ya kuwaunganisha sambamba na kuwezesha ushirikiano baina yao ili kuhuisha viwanda hivyo kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Amiron Medical Equipment Ltd, Bw. Monge Kigezo ameishukuru SANVIN kwa kuwawesha kufikia hatua hiyo kwani kupitia uwekezaji huo itapunguza matumizi ya fedha za kigeni ya manunuzi ya vifaa tiba vilivyokuwa vikinunuliwa nnje ya nchi."Tunashukuru kwa kweli bila SANVIN haya mafanikio yasingekuwepo, shukrani pekee kwakweli tunazitoa kwa Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira wezeshi ya Viwanda binafsi lakini pia kutoa soko"Monge amesema.Ziara hiyo imethibitisha kuwa uwezeshaji unaotolewa kupitia SANVIN Viwanda Scheme una mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa wajasiriamali wa ndani, huku NEEC ikiendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wake ili kufikia malengo ya maendeleo jumuishi na endelevu.Mpaka sasa wanufaika wa Mradi wa SANVIN wamefikia 94 kutoka katika mikoa 13 ambayo ni pamoja na Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya, Geita, Kilimanjaro, Pwani, Njombe, Dodoma, Iringa, Shinyanga, Rukwa na Singida.

Articles similaires

MHE. SIMBACHAWENE ATEMBELEA JENGO JIPYA LA SEKRETARIETI YA AJIRA, ATOA SHUKRANI KWA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 15/Jul 19:38

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa...

MHE. SIMBACHAWENE ATEMBELEA JENGO JIPYA LA SEKRETARIETI YA AJIRA, ATOA SHUKRANI KWA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 15/Jul 19:38

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa...

MCHENGERWA ATAKA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA BARABARA JIMBO LA UKONGA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 19/Jul 18:40

 Na John MapepeleWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa amemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Banana –...

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA (EACOP) UMELETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KWA WANANCHI WA TANGA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 17:03

 📌Wananchi wampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya ujenzi wa Mradi, wafikia...

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA (EACOP) UMELETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KWA WANANCHI WA TANGA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 17:03

 📌Wananchi wampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya ujenzi wa Mradi, wafikia...

KATIBU MKUU MKOMI AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA MAKAZI YA WATUMISHI KIJIJI CHA KIJIWENI

msumbanews.co.tz - 15:16

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wakwanza kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya...

WAZIRI MAVUNDE AKAGUA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA NANE LA MAFUNZO YA UONGEZAJI THAMANI MADINI VITO

msumbanews.co.tz - 22/Jul 15:26

  ▪️Bilioni 33 kukutumika kukamilisha Jengo la ghorofa pacha-TGC Arusha▪️Biashara ya madini kufanyika kwenye Jengo▪️Ni mkakati wa...

BILIONI MBILI KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA ZA TARURA JIJI LA ARUSHA

msumbanews.co.tz - 12/Jul 06:10

Wakala wa Barabra za mijini na Vijini TARURA  wanatarijia zaidi ya bilioni mbili kukamilisha Ujenzi wa Barabara ya TCA Levolisi,CCM,...

Dkt. Biteko- Sekta ya Nishati Ni Uti wa Mgongo wa Maendeleo ya Viwanda Nchini

msumbanews.co.tz - 11/Jul 05:51

 SERIKALI ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua thabiti za kuboresha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya viwanda...

STAMICO YAKABIDHIWA LESENI KUBWA YA UTAFITI NA UCHIMBAJI MADINI ADIMU VILIMA VYA WIGU,MOROGORO

msumbanews.co.tz - 12:59

 Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amekabidhi Leseni ya Utafiti na Uchimbaji Mkubwa wa Madini Adimu na Muhimu ambayo ni ya kimkakati ya Rare...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément