Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMIWaziri Mchengerwa ameeleza azma ya Serikari ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha Mfumo wa Ufundishaji Mubashara (live...
Vous n'êtes pas connecté
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMIWaziri Mchengerwa ameeleza azma ya Serikari ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha Mfumo wa Ufundishaji Mubashara (live teaching) unaanza kutumika nchi nzima ili kumuwezesha mwalimu kutoka katika kituo kimoja kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja wakiwa katika mikoa tofauti.Azma hiyo ya Serikali imeelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, alipofanya ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha ambayo ina kituo (smart class) cha ufundishaji mubashara (live teaching).Waziri Mchengerwa amesema, anatambua kuwa Kibaha Sekondari ni moja ya kituo kinachotegemewa kwa ajili ya ufundishaji mubashara kwani mwalimu anaweza kufundisha akiwa Kibaha Sekondari na wanafunzi nchi nzima wakaudhuria kipindi chake.“Kibaha Sekondari ni lazima muendelee kutumia Mfumo wa Ufundishaji Mubashara kwani niliuzindua mwenyewe jijini Dodoma kwa kuiunganisha Kibaha Sekondari na Dodoma Sekondari na tulijionea namna mfumo unavyofanya kazi na sasa tunataka uende nchi nzima,” Mhe. Mchengerwa alisisitiza.Sanjari na hiyo, Mhe. Mchengerwa amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Rogers Shemwelekwa kwa kuhimiza matumizi ya Mfumo wa Ufundishaji Mubashara katika Shule ya Sekondari Kibaha na kumtaka aendelee kuiwezesha shule hiyo kuwa kituo cha mfano cha ufundishaji mubashara nchini, kwani wakati akiwa Shirika la Elimu Kibaha aliwezesha mfumo huo kufanya kazi.Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa, iwapo miundombinu ya elimu itaendelea kuboreshwa katika Shule ya Sekondari Kibaha, hapo baadae kuna uwezekano Serikali ikafikiria kujenga chuo kikuu katika eneo hilo hilo ambalo shule hiyo ipo ili kutimiza lengo la Rais Samia la kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu.Aidha, Waziri Mchengerwa amempongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Bw. George Kazi kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtaka aendelee kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita wanaendeleza utamaduni wa kupata ufaulu mzuri, na kuongeza kuwa akishindwa kutekeleza jukumu hilo atawajibishwa.Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Bw. George Kazi amemueleza Waziri Mchengerwa kuwa yeye pamoja timu nzima ya walimu anaowaongoza wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kufundisha usiku na mchana ili kutoa ufaulu mzuri kwa wanafunzi wote wanaomaliza Kibaha Sekondari. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Mchengerwa mnamo Februari 07, 2024 alizindua majaribio ya Ufundishaji Mubashara katika Shule ya Sekondari Dodoma, majaribio hayo yameonesha matokeo chanya katika kuongeza ufahamu wa wanafunzi kwenye shule ambazo zina vituo (smart classes) vya Ufundishaji Mubashara (live teaching).
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMIWaziri Mchengerwa ameeleza azma ya Serikari ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha Mfumo wa Ufundishaji Mubashara (live...
Katika mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA, Sajenti Emmanuel kutoka Jeshi la Polisi, kitengo cha Dawati la Jinsia na...
Katika mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA, Sajenti Emmanuel kutoka Jeshi la Polisi, kitengo cha Dawati la Jinsia na...
▪️Bilioni 33 kukutumika kukamilisha Jengo la ghorofa pacha-TGC Arusha▪️Biashara ya madini kufanyika kwenye Jengo▪️Ni mkakati wa...
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wakwanza kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa...
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amekabidhi Leseni ya Utafiti na Uchimbaji Mkubwa wa Madini Adimu na Muhimu ambayo ni ya kimkakati ya Rare...
Na John MapepeleWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa amemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Banana –...
Na WAF, DodomaSerikali ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2024/25 na 2025/26 imetoa jumla ya Dola Milioni 114 sawa na Shilingi Bilioni 298 za...