X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 10/Oct 17:05

SERIKALI IMETOA TRILIONI 3.5 KUWAWEZESHA VIJANA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imefanikiwa kutoa kiasi cha shilingi trilioni 3.5 kufikia mwaka 2024 kwa ajili ya uwezeshaji wa vijana kiuchumi kutoka shilingi bilioni 904 mwaka 2021.Amesema kuwa fedha hizo zimewasaidia vijana kupata mitaji *ambayo ambayo* imewawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na hatimaye kuinua vipato vyao pamoja na uchumi wa Taifa.Amesema hayo leo Ijumaa (Oktoba 10, 2025) Wakati *wa* maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa iliyofanyika mkoani Mbeya. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.”Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imefanya hivyo kwa kutambua kuwa Vijana ni nguvu kazi  na ndiyo msingi wa safari ya maendeleo ya Taifa letu. “Vijana wakipewa nafasi na kuandaliwa ipasavyo, wanaweza kuwa nguzo kuu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs)”.Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa vijana wamekuwa nguzo muhimu ya maendeleo katika sekta mbalimbali nchini na wamechangia kwa kiwango kikubwa katika kilimo, biashara, teknolojia, michezo na sanaa. “Katika nyanja za ubunifu na teknolojia, vijana ndiyo vinara wa matumizi ya teknolojia mpya na majukwaa ya kidijitali, ikiwemo akili mnemba (artificial intelligence) na mifumo ya mawasiliano ya kisasa, Michango yao imekuwa kichocheo cha mabadiliko chanya katika jamii na uchumi wa Taifa.”Pia Mheshimiwa ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha vijana wanashirikishwa kikamilifu katika ngazi zote za maamuzi na si tu kama wanufaika wa sera bali pia kama wabunifu na viongozi wa mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.Akizungumza alipotembelea Banda la VETA , Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Taasisi hiyo pamoja wadau wengine wa elimu kuwapa kipaumbele cha mafunzo Wenye Ulemavu pamoja na kuwaandalia nyenzo muhimu za kujifunzia ili waweze kutumia ujuzi watakaoupata kuongezea kipato.“Baada ya kutembelea Banda hili nimejifunza kwamba wapo vijana Wenye Ulemavu wana ujuzi na vipaji, Wazazi tuwe tayari Kuwatoa watoto wetu Wenye Ulemavu na Taasisi za elimu ziwapokee na kuwapa ujuzi”Kwa Upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa kundi la Vijana na ndiyo maana inawekeza na kuthamini mchango na nguvu zao katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii zetu. “Hii ni rasilimali kubwa ambayo ikielekezwa na ikijengewa uwezo ipasavyo kupitia vipaji walivyonavyo italeta maendeleo endelevu, kujenga taifa shindani na lenye ustawi”.

Articles similaires

MRADI WA WLER WAIBUA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU GONGO LA MBOTO

msumbanews.co.tz - 25/Oct 20:10

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMWANAWAKE wa Kata ya Gongo la Mboto wamehamasishwa kushiriki katika nafasi za uongozi na kujiimarisha kiuchumi...

MICHEZO YALETA MSHIKAMANO NA AFYA KWA WATUMISHI MADINI

msumbanews.co.tz - 18/Oct 13:26

 Wizara ya Madini leo Oktoba 18, 2025, imeshiriki Bonanza la Michezo lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin jijini Dodoma,...

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU KUJENGA KAMPASI MPYA MAKAMBAKO

msumbanews.co.tz - 22/Oct 09:54

 Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Fatma Mode wamefanya ziara ya...

DKT. MATARAGIO AAGIZA VIFAA VYOTE VYA UHAKIKI WA JOTOARDHI ZIWA NGOZI KUFIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 22/Oct 17:36

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni yake Tanzu ya Uendelezaji...

WAKUU WA VITENGO VYA UFUATILIAJI NA TATHMINI WA SEKRETARIETI ZA MIKOA WAJENGEWA UWEZO WA MASUALA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI NCHINI

msumbanews.co.tz - 23/Oct 17:22

 Na Mwandishi WETU, SINGIDAOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeandaa kikao kazi cha siku 3 kilichowakutanisha Wakuu   vitengo vya...

NAMELOK ATOA SOMO NAMNA YA UPIGAJI KURA KWA JAMII YA KIFUGAJI YA KIMASAI

msumbanews.co.tz - 28/Oct 19:06

MJUMBE wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Namelok Sokoine Ametoa somo la elimu ya jinsi ya kupiga kura kwa jamii ya...

NAMELOK ATOA SOMO NAMNA YA UPIGAJI KURA KWA JAMII YA KIFUGAJI YA KIMASAI

msumbanews.co.tz - 28/Oct 19:06

MJUMBE wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Namelok Sokoine Ametoa somo la elimu ya jinsi ya kupiga kura kwa jamii ya...

MRADI WA WLER WALETA MAPINDUZI MAKUBWA YA USAWA WA KIJINSIA CHANIKA

msumbanews.co.tz - 25/Oct 18:36

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMKituo cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Chanika kimeibuka na ajenda ya kuimarisha miundombinu ya shule na uwezo wa...

DCEA Yakamata Tani 10 za Dawa za Kulevya, Yatoa Onyo kwa Wanafunzi na Bodaboda

msumbanews.co.tz - 21/Oct 12:47

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMMamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata watuhumiwa wanne katika eneo la Mlalakuwa,...

VIONGOZI WA DINI SHINYANGA WAIHIMIZA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA KWA AMANI OKTOBA 29

msumbanews.co.tz - 18/Oct 18:22

Na Mapuli Kitina MisalabaViongozi wa Dini mkoani Shinyanga wametoa tamko maalum wakiiasa jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la upigaji...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément