X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

  - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 18/Jul 16:38

TANZANIA NA KENYA WAZINDUA RASMI MAUNGANISHO YA MKONGO WA MAWASILIANO

Mawaziri wa Mawasiliano kutoka Tanzania na Kenya wamezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wa Tanzania unaosimamiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), na mikongo ya baharini ya Mombasa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (ICTA).Uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidigitali wa Kenya, Injinia William Kabogo Gitau, pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania, Mhe. Jerry Silaa. Mawaziri hao wamesisitiza kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria, ikilenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya uhakika, pamoja na kupunguza changamoto za kukatika kwa mtandao.Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Gitau amesema: “Jambo la msingi ni ushirikiano wa dhati kati ya nchi zetu mbili. Ni muhimu kuhakikisha tunatunza miundombinu hii ya kimkakati ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababisha kukatika kwa umeme na mtandao. Pia tuendelee kuimarisha mahusiano yetu kwa manufaa ya pande zote.”Kwa upande wake, Mhe. Jerry Silaa alisema kuwa ujenzi wa miundombinu ya pamoja ya mawasiliano kati ya nchi washirika ni wajibu wa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya kikanda. “Kuna faida kubwa ya kuwa na maunganisho mengi ya mikongo ya mawasiliano. Hii husaidia kuwepo kwa mtandao wa uhakika, unaotegemewa hata wakati wa changamoto za kiufundi katika njia moja ya mawasiliano,” alisema Silaa.Mkongo huo tayari umeanza kufanya kazi nchini Kenya, hatua inayowezesha huduma za intaneti na mawasiliano kusambaa kwa kasi zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Uzinduzi huu unaashiria mafanikio makubwa katika juhudi za kuunganisha ukanda huu kidigitali na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Articles similaires

TANZANIA NA KENYA WAZINDUA RASMI MAUNGANISHO YA MKONGO WA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 18/Jul 16:38

Mawaziri wa Mawasiliano kutoka Tanzania na Kenya wamezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wa Tanzania unaosimamiwa na...

WASHIRIKA WA MAENDELEO KUCHANGIA SH. BILIONI 161 MFUKO WA AFYA WA PAMOJA

msumbanews.co.tz - 19/Jul 06:26

 Na. Peter Haule, WF, Dar es SalaamSerikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund),...

WIZARA YA FEDHA YATWAA TUZO MAONESHO YA 49 YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 07/Jul 16:34

 Wizara ya Fedha imeibuka na tuzo ya Mshindi wa Tatu wa jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es...

WASHIRIKI 700 KUKUTANA MKOANI ARUSHA KATIKA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA MWAKA WA JUMUIYA YA WATAALAMU WA RASILIMALI WATU NA UTAWALA (TAPA-HR)

msumbanews.co.tz - 18/Jul 20:58

Jumla ya Washiriki 700 kutoka taasisi mbalimbali za Tanzania bara na Visiwani,wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa Jumuiya ya...

Dkt. Biteko- Sekta ya Nishati Ni Uti wa Mgongo wa Maendeleo ya Viwanda Nchini

msumbanews.co.tz - 11/Jul 05:51

 SERIKALI ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua thabiti za kuboresha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya viwanda...

HATI MILKI ZA ARDHI 1,176 ZATOLEWA MAONESHO YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 08:41

Na Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jumla ya Hati Milki za Ardhi 1,176 wakati wa Maonesho ya Kimataifa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément