X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

  - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 16/Jul 08:41

HATI MILKI ZA ARDHI 1,176 ZATOLEWA MAONESHO YA SABASABA

Na Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jumla ya Hati Milki za Ardhi 1,176 wakati wa Maonesho ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yaliyomalizika mwishoni mwa wiki. Katika maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu ya "Fahari ya Tanzania" Wizara ya Ardhi imetoa huduma mbalimbali ikiwemo hati milki za ardhi kwa wamiliki waliokamilisha taratibu za umiliki pamoja na utatuzi wa changamoto za sekta ya ardhi.  Akizungumza wakati wa hitimisho la maonesho hayo jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam anayeshughulikia wilaya ya Ilala na Temeke Rehema Mwinuka alisema, kati ya hati hizo 1,176, hati 1,040 zimetolewa kwa wamiliki wa mkoa wa Dar es Salaam, 68 Pwani na 68 ni kwa mkoa wa Pwani. Kwa mujibu wa Rehema, wizara ya Ardhi katika maonesho hayo ya Sabasaba ilihudumia zaidi ya wananchi 1,616 waliofika kuhitaji huduma za sekta ya ardhi katika maeneo mbalimbali. "Katika maonesho ya mwaka huu wizara yetu ilijipanga kutoa huduma mbalimbali na imefanikiwa kuwahudumia zaidi ya wananchi 1,616 huku hati 1,176 zikitolewa" alisema Rehema. Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliofika Banda la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi walionesha kuridhishwa na huduma zilizokuwa zikitolewa wakati wote wa maonesho na kusisitiza umuhimu wa wizara ya Ardhi kuandaa huduma ya pamoja (One Stop Center) ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za sekta ya ardhi. Walitolea mfano wa huduma ya utoaji Hati Milki za Ardhi pamoja na ukadiriaji kodi ya pango la ardhi kuwa, ni moja ya huduma iiliyopatikana kwa haraka jambo linaloonesha kuwa, wizara ilijipanga katika maonesho hayo Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Mhe. Aisha Bade ambaye ni mmoja wa waliopata hati milki ya ardhi katika maonesho hayo alisema, wizara ya Ardhi kwa sasa imebadilika kwani huko nyuma kupata hati ilichukua zaidi ya mwaka. "Niwapongeze wizara ya ardhi kwa hatua mliyofikia, huko nyuma kupata hati milki ya ardhi ni 'issue' lakini leo nimeipata hati yangu ndani ya muda mfupi, hongereni sana" alisema.  Naye Muigizaji wa sinema za kitanzania (Bongo Movie) Richie Mtambalike ameipongeza wizara ya ardhi kwa kutoa huduma za papo hapo hasa utoaji wa hati milki za ardhi katika maonesho ya kimataifa ya sabasaba. "Niishukuru Wizara ya Ardhi kwa kutuletea huduma hapa katika maonesho maana kwa upande wangu nimefanikiwa kupata hati milki ya arhi hapa hapa" alisema. Katika maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu Wizara ya Ardhi ilitoa huduma za sekta ya ardhi kwa mkoa wa Dar es salaam ikihusisha manispaa za Kinondoni, Ubungo, Kigamboni, Ilala na Temeke, mkoa wa Pawani pamoja na Dodoma. Vile vile, elimu kuhusiana na masula ya Sekta ya Milki, Urasimishaji Makazi Holela, Mbaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya pamoja na namna ya kujiunga na Chuo cha  Ardhi Morogoro (ARIMO) katika masomo kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada zilitolewa. 

Articles similaires

HATI MILKI ZA ARDHI 1,176 ZATOLEWA MAONESHO YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 08:41

Na Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jumla ya Hati Milki za Ardhi 1,176 wakati wa Maonesho ya Kimataifa...

TBA YAWASHUKURU WANANCHI, YAAHIDI MABORESHO ZAIDI YA HUDUMA

msumbanews.co.tz - 15/Jul 06:59

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daudi Kondoro, ametoa shukrani kwa wananchi wote waliotembelea Banda la TBA katika...

DKT.YONAZI AIPONGEZA OFISI YA WAZIRI MKUU MAONESHO SABASABA

msumbanews.co.tz - 18/Jul 13:20

 Na Mwandishi wetu- DodomaKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza watumishi wa Ofisi ya...

MWAIPAJA: TUTAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAJUKWAA MENGINE BAADA YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 14/Jul 04:49

 Na. Peter Haule na Joseph Mahumi,WF, Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amewataka...

WASHIRIKA WA MAENDELEO KUCHANGIA SH. BILIONI 161 MFUKO WA AFYA WA PAMOJA

msumbanews.co.tz - 19/Jul 06:26

 Na. Peter Haule, WF, Dar es SalaamSerikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund),...

“LENGO KUU LA KUSHIRIKI MAONESHO HAYA NI KUTOA ELIMU KWA UMMA” – MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

msumbanews.co.tz - 10/Jul 18:08

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amefanya ziara ya kutembelea maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément