Na Munir Shemweta, WANMM Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza ya Ardhi nchini ambaye ni Naibu Msajili wa...
Vous n'êtes pas connecté
Na Munir Shemweta, WANMM Serikali imeitaka Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza kuhakikisha madalali wanazingatia kanuni katika kufanya utekelezaji amri zinazotolewa na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya. Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai 2025 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera kwa niaba ya Waziri wa Ardhi Mhe. Deogratius Ndejembi wakati Kamati ya kusimamia uteuzi na nidhamu za Madalali wa Mabaraza ya Ardhi nchini ilipokwenda kujitambulisha kwa Wizara. Kupitia taarifa ya Waziri wa Ardhi, Bi Lucy amesema, kanuni za madalali zimeweka marufuku mbalimbali kwa madalali kama vile marufuku ya kutekeleza amri nyakati za usiku au kabla hakujapambazuka vizuri pamoja na siku za mwisho wa wiki. Aidha, kanuni imetaka pia madalali kuepuka kutweza utu wa wale ambao amri zimetolewa dhidi yao hususan utekelezaji unaohusishwa wagonjwa wazee, akina mama na watoto. "Kwa kuwa kanuni za uteuzi na nidhamu za madalali wa Mabaraza ya Ardhi ya mwaka 2003 zimeweka utaratibu mzuri wa kufanya kazi katika mazingira haya, tafadhali zingatieni kanuni hizi muhimu ambazo serikali imeweka ili kulinda utu na heshima za wananchi" amesema. Akielezea kuhusu madalali wasio na leseni za kutekeleza amri za mabaraza ya ardhi, kujichukulia sheria mkononi sambamba na kutekeleza majukumu yasiyo ya kwao, amesema, vitendo hivyo ni kinyume cha sheria na kwa kuwa kamati ina muakilishi kutoka wizara ya mambo ya ndani ni matumaini yake madalali wa aina hiyo watakapokiuka sheria za nchi watachukuliwa hatua stahiki. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza Suzan Kihawa ameahidi kamati yake kufanya kazi kwa bidiii huku wakizingatia kanuni na taratibu zinafuatwa na madalali katika kutekeleza majukumu yake. ‘’Mhe Naibu Katibu Mkuu nikuahidi kamati yetu itahakikisha madalali wanazingatia kanuni katika kufanya utekelezaji wa amri zinazotolewa na mabaraza ya ardhi na Nyumba ya wilaya’’ amesema Suzan Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yenye jukumu la kusikiliza na kuamua mashauri yanayotokana na migogoro ya umiliki wa ardhi yanahitimisha jukumu hilo kwa kuwatumia madalali wa mabaraza kutekeleza amri zinazotolewa pale mdaawa aliyeshindwa kesi anaokaidi kutii amri husika. Kamati ya uteuzi na nidhamu za madalali wa Mabaraza ya Ardhi ina jumla ya wajumbe sita wanaoteuliwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo katibu wake ni Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya. Wajumbe wa Kamati ni wataalamu waandamizi wanaowakilisha wizara na taasisi ambazo kwa namna moja ama nyingine zinahusika katika utatuzi wa migogoro ya umiliki wa ardhi. Muundo wa kamati hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 28B cha sheria ya mahakama za utatuzi wa migogoro ya ardhi Sura ya 216.
Na Munir Shemweta, WANMM Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mabaraza ya Ardhi nchini ambaye ni Naibu Msajili wa...
Na Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jumla ya Hati Milki za Ardhi 1,176 wakati wa Maonesho ya Kimataifa...
Na Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jumla ya Hati Milki za Ardhi 1,176 wakati wa Maonesho ya Kimataifa...
*Na Mwandishi wetu- RUKWAMkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya, Mhe. Nyakia Ally Chirukile, amezindua...
*Na Mwandishi wetu- RUKWAMkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya, Mhe. Nyakia Ally Chirukile, amezindua...
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameshiriki kikao cha 58 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Biashara na Uwekezaji...
Na Munir Shemweta, WANMM Serikali imesema kuwa, mafunzo ya uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Burundi yanalenga kujenga uelewa wa...
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi,WF, Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amewataka...
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi,WF, Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amewataka...
21 Julai, 2025, Bagamoyo, PwaniNaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Dkt. Hussein Mohamed Omar ametembelea Wakala wa...