Na Mwandishi wetu- DodomaKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza watumishi wa Ofisi ya...
Vous n'êtes pas connecté
Na Mwandishi wetu- DodomaKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo ya Taifa.Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo tarehe 18 Julai, 2025 Ofisini kwake jijini Dodoma akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Bw. Conrad Milinga iliyotolewa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akifungua Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025.Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kupokea tuzo kumeongeza motisha katika ushiriki wa maonesho yajayo makubwa ya Kimataifa ya Sabasaba na kutambua mchango wa Ofisi hiyo iliyoutoa kwa wananchi katika kipindi chote cha maonesho hayo na kutambua huduma ianayotolewa kwa wananchi.“Ofisi ya Waziri Mkuu imefurahi sana kupokea tuzo hii kama ishara ya kutambua ushiriki wetu na mchango ambao Ofisi yetu inatoa kwa wananchi hivyo tunaamini ushiriki wetu unaofuata utakuwa wa viwango vya juu sana,” Alisema Dkt. Yonazi.Pia aliishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inazofanya chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambayo ndio mratibu wa Maonesho kwa kuhakikisha maonesho hayo yanaleta tija na mageuzi makubwa katika sekta ya kiuchumi kwa wananchi na Kimataifa.“Tunazishukuru sana Taasisi mbalimbali ambazo tumeshirikiana nazo na viongozi ambao wameendelea kutupa maelekezo yaliyowezesha kufanya vizuri katika maonesho hayo na tunaamini kwamba tutaendelea kuwa washindi au hata washindi wa jumla,”Alishukuru.Ikumbukwe Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi tarehe 07 Julai, 2025 na kufungwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanja vya maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 13, 2025.
Na Mwandishi wetu- DodomaKatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza watumishi wa Ofisi ya...
Na. Peter Haule, WF, Dar es SalaamSerikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund),...
Na. Peter Haule, WF, Dar es SalaamSerikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund),...
Na Mwandishi wetu- MorogoroSerikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepongezwa kwa kuendelea kufanya mageuzi...
Na Mwandishi wetu- MorogoroSerikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepongezwa kwa kuendelea kufanya mageuzi...
Na Mwandishi wetu- DODOMAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi amefanya ukaguzi wa maandalizi ya...
Na WAF - Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuchukua uamuzi wa...
📌Rais Samia mgeni rasmi Maadhimisho ya Mashujaa kesho📌Atoa wito kwa wananchi kushiriki Maadhimisho ya MashujaaNa Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na...
📌Rais Samia mgeni rasmi Maadhimisho ya Mashujaa kesho📌Atoa wito kwa wananchi kushiriki Maadhimisho ya MashujaaNa Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na...
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Bw. Ali Goktug IPEK,wakibadilishana Mkataba mara...