▪️Bilioni 33 kukutumika kukamilisha Jengo la ghorofa pacha-TGC Arusha▪️Biashara ya madini kufanyika kwenye Jengo▪️Ni mkakati wa...
Vous n'êtes pas connecté
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Bw. Ali Goktug IPEK,wakibadilishana Mkataba mara baada ya kusaini Azimio la Kamati ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati ya Tanzania na Uturuki hafla iliyofanyika leo Julai 23,2025 jijini jijini Dar es Salaam. Na.Mwandishi Wetu SERIKALI ya Tanzania imeweka malengo makubwa ya kibiashara kwa kushirikiana na Uturuki, ikilenga kufikia thamani ya biashara ya Dola za Kimarekani bilioni 1. Hii ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uchumi wa nchi kupitia diplomasia ya kiuchumi na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Uturuki. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kusaini Azimio la Kamati ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati ya Tanzania na Uturuki, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,amesema kuwa ushirikiano huo unalenga kuzalisha bidhaa bora na kukuza sekta ya viwanda, kilimo na madini kwa masoko ya kimataifa. “Kupitia timu ya wataalamu na ushirikishwaji wa sekta binafsi, tutashirikiana katika biashara kama lango kuu la fursa,” amesema Dkt. Jafo. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2024, biashara kati ya Tanzania na Uturuki ilikuwa Dola milioni 284, ambapo Uturuki iliuza bidhaa zenye thamani ya Dola milioni 217 kwa Tanzania, ikionesha fursa kubwa bado hazijatumika kikamilifu. Waziri Jafo ameeleza kuwa mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Uturuki yameimarika kwa kasi, hasa baada ya kufunguliwa kwa balozi za nchi hizo mwaka 2009 na 2017 mtawalia. Amesema kuwa ziara za viongozi wakuu wa mataifa haya, ikiwemo ile ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan nchini Tanzania na ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Uturuki mwaka 2024, zimekuwa kichocheo kikubwa cha ushirikiano huu. Vilevile,amesema kuwa makampuni ya Kituruki yamekuwa sehemu ya miradi mikubwa ya maendeleo nchini, kama vile ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ambayo imeleta ajira na fursa mpya kwa Watanzania. “Makampuni ya Uturuki, hasa kwenye SGR, yameweza kufanya biashara ambayo italeta fursa nyingi kwa wananchi wetu,” amesema Waziri Jafo. Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Bw. Ali Goktug IPEK, ameeleza kuwa JTC ni jukwaa muhimu litakalosaidia kuondoa vikwazo vya kibiashara, kurahisisha michakato ya biashara na kuvutia uwekezaji mpya. “Kamati ya Pamoja ya Biashara itakuwa jukwaa lenye nguvu la kuondoa vikwazo, kukuza uwekezaji, na kufungua fursa mpya kwa mataifa yote mawili,” ameeleza Balozi Goktug. Ameongeza kuwa Uturuki imejipanga kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, kilimo, nishati na teknolojia, huku akisisitiza dhamira ya kuimarisha maendeleo ya pamoja chini ya uongozi wa Rais Erdoğan na Rais Samia. Kwa ujumla, Tanzania ina matumaini makubwa kuwa ushirikiano huu utafungua ukurasa mpya wa maendeleo ya kiuchumi, ajira na mafanikio kwa wananchi wake. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla ya kusaini Azimio la Kamati ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati ya Tanzania na Uturuki iliyofanyika leo Julai 23,2025 jijini Dar es Salaam. Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Bw. Ali Goktug IPEK,wakati wa hafla ya kusaini Azimio la Kamati ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati ya Tanzania na Uturuki iliyofanyika leo Julai 23,2025 jijini Dar es Salaam.
▪️Bilioni 33 kukutumika kukamilisha Jengo la ghorofa pacha-TGC Arusha▪️Biashara ya madini kufanyika kwenye Jengo▪️Ni mkakati wa...
Mawaziri wa Mawasiliano kutoka Tanzania na Kenya wamezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wa Tanzania unaosimamiwa na...
Mawaziri wa Mawasiliano kutoka Tanzania na Kenya wamezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wa Tanzania unaosimamiwa na...
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameshiriki kikao cha 58 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Biashara na Uwekezaji...
Na. Peter Haule, WF, Dar es SalaamSerikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund),...
Na. Peter Haule, WF, Dar es SalaamSerikali ya Tanzania na washirika wa Maendeleo wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund),...
Na Munir Shemweta, WANMM Serikali imesema kuwa, mafunzo ya uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Burundi yanalenga kujenga uelewa wa...
Airtel Tanzania leo imezindua rasmi huduma ya Airtel Chapakazi, suluhusho jipya lililoundwa kuchochea ukuaji wa wajasiriamali na wafanyabiashara...
Airtel Tanzania leo imezindua rasmi huduma ya Airtel Chapakazi, suluhusho jipya lililoundwa kuchochea ukuaji wa wajasiriamali na wafanyabiashara...
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMSHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) wamesaini mkataba wa makubaliano na Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways)...