X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 16/Jul 12:00

DKT. YONAZI AIPONGEZA SERIKALI MAGEUZI SEKTA YA KILIMO

 Na Mwandishi wetu- MorogoroSerikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepongezwa kwa kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji, tija na faida kwa wakulima na wananchi kwa ujumla.Pongezi hizo zimetolewa na, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akifungua warsha kuhusu kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Kilimo  leo tarehe 16 Julai, 2025 katika Ukumbi wa Mbaraka Mshee - Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, mkoani Morogoro.Dkt. Yonazi alisema, hatua hiyo ni kutokana na Serikali kuongeza najeti ya Kilimo kwa miaka mitatu mfululizo kutoka bilioni 294 (2022/2023) hadi  trilioni 1.241 (2025/2026) ambapo katika kufanikisha hilo Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imezindua Programu na Mipango ya kufanikisha malengo hayo ambayo ni pamoja na Programu ya BBT, Agenda 10/30 na Agricultural Transformation Master Plan.“Ninapenda kumshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuboresha muundo wa Taasisi za Umma na kuanzisha Idara ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu na Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini katika ngazi zote nchini kwa lengo la kupima utendaji wa Serikali,” alisema Dkt. Yonazi.Pia aliongeza kwamba, warsha hiyo itakayofanyika kwa siku tano itawezeshwa na  wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  kwa kushirikiana na Mtaalam Mbobezi kutoka Benki ya Dunia kuhusu dhana mbalimbali zikiwemo muundo wa kitaasisi wa Ufuatiliaji na Tathmini nchini, Mwongozo Elekezi wa Mwongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali (M&E Operational Manual).“Mpango mwingine ni  Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango kazi wa Mwaka wa Wizara na Taasisi (M&E Plan), Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (M&E Strategy) na Moduli ya kupima utendaji wa Wizara na Taasisi husika (M&E Performance Model). Aidha, ni muhimu kupima hali ya utayari wa kila Wizara na Taasisi zake,” alieleza .Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu imekasimiwa jukumu la kuratibu, kufuatilia, kutathmini na kupima utendaji wa serikali nchini hivyo ofisi imeendelea kuratibu shughuli hizo kwa kuandaa na kuwasilisha nyaraka muhimu zitakazowezesha ubora na ufanisi wa kazi za ufuatiliaji na tathmini. “Ni muhimu kuvisimamia vitengo vyenu kutekeleza majukumu yao kwa kufuata miongozo ili kazi zetu ziwe na ubora unaotakiwa. Aidha, ni matarajio yangu kuwa nyaraka hizo zitawaongoza kuandaa nyaraka elekezi na tendaji kwa kuzingatia muktadha wa Wizara yenu ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yenu,” alibainisha.Aidha, Dkt. Yonazi aliwasihi washiriki wa warsha hiyo  kujadili masuala yote ikiwemo changamoto zinazoweza kusababisha kuwa na utekelezaji usioridhisha katika Wizara mbalimbali na Taasisi zake ikiwemo Wizara ya Kilimo pamoja na kupendekeza namna bora ya kuondokana na changamoto hizo.MWISHO

Articles similaires

NISHATI YAWASILISHA MIPANGO YA KIMKAKATI KUTEKELEZA DIRA YA TAIFA 2050

msumbanews.co.tz - 07/Oct 09:16

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, amekutana na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango wakiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji...

MICHEZO YALETA MSHIKAMANO NA AFYA KWA WATUMISHI MADINI

msumbanews.co.tz - 13:26

 Wizara ya Madini leo Oktoba 18, 2025, imeshiriki Bonanza la Michezo lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin jijini Dodoma,...

FCC KUJIKITA KUIMARISHA UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA KUPITIA MFUMO WA TANOGA

msumbanews.co.tz - 17/Oct 04:23

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Serera,akizungumza  leo, Oktoba 16, 2025, wakati wa ziara ya pamoja kati ya...

MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU :MVUTANO WA AINA YAKE AFRIKA

msumbanews.co.tz - 06/Oct 08:58

  Mijadala kuhusu uhuru wa maamuzi na maadili barani Afrika inazidi kupamba moto, na Tanzania iko katikati ya mvutano wa kitamaduni wa kimataifa....

NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AFUNGUA KIKAO KAZI CHA TAASISI ZA KISHERIA

msumbanews.co.tz - 16/Oct 12:28

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Samwel M. Maneno, amesema serikali imejipanga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi zake za kisheria ili kuongeza...

SERIKALI YAENDESHA WARSHA KUJENGA USHIRIKIANO NA WASHIRIKA WA MAENDELEO

msumbanews.co.tz - 14/Oct 07:39

 Na. Eva Ngowi -Wizara ya Fedha, Dar es Salaam Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar...

SERIKALI YAENDESHA WARSHA KUJENGA USHIRIKIANO NA WASHIRIKA WA MAENDELEO

msumbanews.co.tz - 14/Oct 07:39

 Na. Eva Ngowi -Wizara ya Fedha, Dar es Salaam Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar...

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO WIZARA YA MADINI

msumbanews.co.tz - 07/Oct 11:48

 Aitaka ifuatilie kampuni zilizoshika maeneo bila kuyaendelezaAipongeza kampuni ya Huaer International kwa uwekezaji.Asisitiza uwekezaji  huo ni...

WAKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO WAFANYA MAPITIO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

msumbanews.co.tz - 06:33

 Serikali kupitia Wizara ya Fedha, imefanya kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta,...

SERIKALI IMETOA TRILIONI 3.5 KUWAWEZESHA VIJANA-MAJALIWA

msumbanews.co.tz - 10/Oct 17:05

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imefanikiwa kutoa kiasi cha shilingi trilioni 3.5 kufikia mwaka 2024 kwa ajili ya uwezeshaji wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément