Awataka Wakandarasi kuongeza kasi ili Miradi ikamilike kwa wakatiAsema lengo la TANESCO ni kuhakikisha inamudu mahitaji ya wateja wakeMkurugenzi...
Vous n'êtes pas connecté
Awataka Wakandarasi kuongeza kasi ili Miradi ikamilike kwa wakatiAsema lengo la TANESCO ni kuhakikisha inamudu mahitaji ya wateja wakeMkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange Julai 18, 2025 amefanya ziara ya kuagua maendeleo ya Miradi ya umeme ukiwemo wa Njia ya kusafirisha umeme kutoka Zuzu hadi Mbande, Mradi wa kusambaza umeme ardhini katika mji Serikali na Mradi wa Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mjini Mkoani Dodoma.Bw. Twange ameelezea maendeleo ya Mradi wa njia ya kusambaza umeme wa Msongo wa Kilovolti 33 kutoka Mbande hadi Zuzu kwamba umefikia asilimia 48.35 huku Mradi wa usambazaji wa umeme ardhini kwenye mji wa Serikali Ihumwa ukifikia asilimia 64 ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 50.09 ambapo amewataka Wakandarasi kuongeza kasi ili Miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ianze kuwahudumia wananchi.Mkurugenzi Mtendaji huyo pia amekagua maendeleo ya Mradi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mjini Dodoma ambacho kimefikia zaidi ya asilimia 80 na kinatarajia kukamilika rasmi mwanzoni mwa mwezi Septemba Mwaka huu.‘’Kituo cha kupokea umeme cha mjini kimefikia zaidi ya asilimia 80, nataka kuwaeleza kuwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa Kituo hiki kitakamilika. Kituo hiki kitatupa uwezo wa kuwasambazia umeme wateja wetu walioko Katikati ya mji kwa kuwa kituo kilichokuwepo awali kilizidiwa na tunachotaka ni kumudu mahitaji ya wateja wetu, alifafanua Bw. Twange.Aidha, Bw. Twange amesema licha ya changamoto za kifedha zilizojitokeza kwa baadhi ya miradi amewapongeza wasimamizi wa Miradi kutoka TANESCO na Wakandarasi ambapo ameeleza kuwa kukamailika kwa miradi hiyo kutachangia upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo Jirani ya Mkoa wa Morogoro.
Awataka Wakandarasi kuongeza kasi ili Miradi ikamilike kwa wakatiAsema lengo la TANESCO ni kuhakikisha inamudu mahitaji ya wateja wakeMkurugenzi...
📌Wananchi wampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya ujenzi wa Mradi, wafikia...
📌Wananchi wampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya ujenzi wa Mradi, wafikia...
Afisa Uhusiano ,Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme (TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro Bi Mwanaisha Mbita akikabidhji jiko la umeme kwa familia ya...
Afisa Uhusiano ,Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme (TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro Bi Mwanaisha Mbita akikabidhji jiko la umeme kwa familia ya...
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wakwanza kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya...
Na WAF - Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuchukua uamuzi wa...
▪️Bilioni 33 kukutumika kukamilisha Jengo la ghorofa pacha-TGC Arusha▪️Biashara ya madini kufanyika kwenye Jengo▪️Ni mkakati wa...
📌Vinalenga kupunguza kasi ya Mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanzania📌Ujenzi wafikia asilimia 50📌 Mabomba ya kipenyo cha inchi...
📌Vinalenga kupunguza kasi ya Mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanzania📌Ujenzi wafikia asilimia 50📌 Mabomba ya kipenyo cha inchi...