X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

  - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 07/Jul 14:49

WANANCHI WAISHUKURU WIZARA YA FEDHA KWA KUWAFUNGUA MACHO

 Na. Peter Haule na Joseph Mahumi ,WF, Dar es Salaam Wizara ya Fedha imeendelea kupongezwa kwa utoaji wa elimu yenye uhalisia na maisha ya wananchi katika masuala ya fedha na uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na matumizi bora ya fedha katika kuchochea maendeleo.Hayo yameelezwa na ujumbe wa Shirika la World Vision Tanzania Mkoa wa Tanga wa mradi wa utunzaji mazingira, ukiongozwa na Bw. Swalehe Mwachuo, ulipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Bw. Mwachuo alisema kuwa wamevutiwa na elimu kuhusu Sera za Fedha na elimu ya huduma ndogo ya fedha ambayo inauhalisia kwa wajumbe wengi wa mradi huo na maeneo walikotoka. Alisema kuwa, ujumbe uliotembelea Banda la Wizara ya Fedha umetoka Mkoani Tanga katika Wilaya za Mkinga, Pangani, Handeni na Kilindi ambao umekuja kupata elimu ya kazi zinazofanywa na Wizara ya Fedha hususani zilizo na manufaa ya moja kwa moja kwa wajumbe hao.Alisema wajumbe hao watapeleka taarifa kwa wananchi wengine kuhusu Sera za fedha na namna ya kuepukana na mikopo umiza, kukopa kwa malengo na kutotumia fedha za mikopo kwenye matumizi yasiyo na faida.Bw. Mwachuo alisema kuwa wamejifunza kuwa fedha za mkopo sio za mkopaji bali faida ndio ya mkopaji hivyo ni vema kutumia fedha ya mkopo kuzalisha ili kupata faida.Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kupitia Idara na Vitengo lakini pia Taasisi zilizo chini ya Wizara, wanaendelea kuwakaribisha watanzania kufika katika Banda la Wizara hiyo ili waweze kuwahudumia. 

Articles similaires

MWAIPAJA: TUTAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAJUKWAA MENGINE BAADA YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 14/Jul 04:49

 Na. Peter Haule na Joseph Mahumi,WF, Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amewataka...

MWAIPAJA: TUTAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAJUKWAA MENGINE BAADA YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 14/Jul 04:49

 Na. Peter Haule na Joseph Mahumi,WF, Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amewataka...

REA YAJIZATITI KUFIKISHA LENGO LA TAIFA KWENYE NISHATI SAFI YA KUPIKIA

msumbanews.co.tz - 08/Jul 08:14

 📌Mkurugenzi Mkuu REA abainisha hatua zinazochukuliwa 📌Amshukuru Rais Samia kwa kuwezeshaMkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),...

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA (EACOP) UMELETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KWA WANANCHI WA TANGA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 17:03

 📌Wananchi wampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya ujenzi wa Mradi, wafikia...

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA (EACOP) UMELETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KWA WANANCHI WA TANGA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 17:03

 📌Wananchi wampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio ya ujenzi wa Mradi, wafikia...

HATI MILKI ZA ARDHI 1,176 ZATOLEWA MAONESHO YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 08:41

Na Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jumla ya Hati Milki za Ardhi 1,176 wakati wa Maonesho ya Kimataifa...

HATI MILKI ZA ARDHI 1,176 ZATOLEWA MAONESHO YA SABASABA

msumbanews.co.tz - 16/Jul 08:41

Na Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jumla ya Hati Milki za Ardhi 1,176 wakati wa Maonesho ya Kimataifa...

EWURA YAPEWA KONGOLE NA MKUU WA WILAYA YA ILEJE KWA KUELIMISHA WADAU WA MAFUTA NA GESI

msumbanews.co.tz - 12/Jul 17:47

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo, tarehe 12 Julai 2025 imeendesha semina ya kuwajengea uelewa wadau wa mafuta na gesi ya...

BODI YA NEEC YATEMBELEA WANUFAIKA WA SANVIN

msumbanews.co.tz - 19/Jul 12:20

NA EMMANUEL MBATILO, PWANIMWENYEKITI wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Profesa Aurelia Kamuzora amesema kutokana na...

RC DKT BATILDA BURIAN APOKEA VIFAA VITAKAVYOTUMIKA KWENYE MRADI WA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI WA HATIFUNGAJI TANGA

msumbanews.co.tz - 11:41

 Na Oscar Assenga,TANGAMKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amewataka wakandarasi watakaohusika katika utekelezaji wa mradi wa hatifungani...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément