X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 14/Feb 09:02

SERIKALI YAJIDHATITI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO – DKT BITEKO

 📌 Anadi soko la mazao jamii ya mikunde India📌 Mnada mazao ya kunde mtandaoni waboresha biashara ya kimataifa📌 Biashara kati ya Tanzania na India kufikia dola bilioni 7.9*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ya Tanzania imejidhatiti kuboresha na kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuja na mipango kadhaa yenye lengo la kuongeza fursa kwa wakulima nchini.Dkt. Biteko amesema hayo jijini New Delhi, India wakati akishiriki mkutano kuhusu masuala ya mazao jamii ya mikunde.“Tunaongeza uwekezaji katika utafiti na kuboresha upatikanaji wa teknolojia za kisasa za kilimo ambapo kila afisa wa ugani nchini amepewa vifaa vyote muhimu ikiwemo pikipiki na kompyuta ili kutoa huduma nzuri na kwa wakati kwa wakulima wetu.” Amesema Dkt. BitekoAmesema Serikali pia imeboresha shughuli za usafirishaji wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kurahisisha michakato ya uuzaji mazao "Tanzania inaendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambayo itaimarisha usafirishaji wa bidhaa yenye urefu wa takribani kilomita 500 kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Dodoma ambayo imekamilika na na inatumika.Vilevile, amesema kupitia mradi wa BBT (Building a Better Tomorrow) Serikali imewezesha vijana kwa kuwapa ardhi, fedha na upatikanaji wa masoko sambamba na kuongeza huduma za kifedha za kidijitali.Aidha, Dkt. Biteko amesema “India ni soko muhimu kwa mazao jamii ya kunde kutoka Tanzania na tunaweza kupata mafanikio makubwa zaidi. Leo nawaalika wawekezaji kutoka India na nchi nyingine duniani kuja kuwekeza katika sekta ya kilimo ya Tanzania kuanzia uzalishaji wa kisasa wa soya hadi uwekezaji katika mifumo ya usimamizi wa mavuno,”Akizungumzia maendeleo ya sekta mazao jamii ya mikunde, amesema kuwa mwaka 2023, Tanzania ilizalisha takriban tani 250,000 za mbaazi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 56 ikilinganishwa na mwaka 2018.Inakadiriwa ifikapo mwaka 2030 Tanzania itakuwa na ukuaji mkubwa katika Pato la Taifa kupitia Kilimo, ambapo mauzo ya maharage mekundu, mbaazi na choroko yanatarajiwa kufikia dola bilioni 1.47, dola milioni 84 na dola milioni 115. Aidha, ili kufikia uwezo huo, Tanzania imeweka mikakati ya kukuza sekta ya mazao jamii ya kunde kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa wakulima kusajiliwa, kuboresha mbinu za kilimo na teknolojia, kuhakikisha ubora na viwango vya mazao kulingana na mahitaji ya soko.Pamoja na hayo Dkt. Biteko amesema “Mazao jamii ya kunde nchini Tanzania yanauzwa kupitia mnada wa mtandaoni ambao unatoa fursa kwa wafanyabiashara kupata taarifa kuhusu mizigo iliyohifadhiwa katika ghala lililosajiliwa,”Amesisitiza “Mfumo huu unahakikisha uwazi, ufuatiliaji na ufanisi katika biashara ya kimataifa. Mwaka 2024 pekee kupitia mfumo huu, wakulima wa Tanzania walipata zaidi ya dola milioni 91.31 kutoka katika biashara ya mbaazi, dengu na maharagwe ya soya, ubunifu huu si tu unaimarisha ushindani wetu bali pia unafungua fursa mpya za ushirikiano,”Kufuatia hali hiyo,kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kimeongezeka na kufikia dola bilioni 7.9 kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Pia, mwaka 2023 mauzo ya mbaazi kutoka Tanzania kwenda India yalifikia tani 186,447 yenye thamani ya dola milioni 139.1

Articles similaires

TANZANIA YAPONGEZWA KWA UKUAJI MZURI WA UCHUMI NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:23

 Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, DodomaWashirika wa Maendeleo nchini wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa maendeleo mbalimbali hususan...

Dkt. Diallo: Taasisi za Kilimo zibadili Mtazamo, zihamasishe Kilimo Biashara kwa Tija"

msumbanews.co.tz - 20/Feb 06:43

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo, amezihimiza taasisi za kilimo nchini kubadili mbinu za...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 PATO LA SERIKALI KWA KIPINDI CHA MIAKA 4

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:44

Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido akitoa taarifa ya utendaji wa Barrick na Twiga kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 SERIKALINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:23

 • Yachangia Zaidi ya Shilingi Trilioni 11 katika Uchumi wa Tanzania• Gawio la Zaidi ya Shilingi Bilioni 412 latolewa kwa SerikaliKampuni ya...

MAWAZIRI WAKUTANA KUJADILI UCHUMI WA BULUU

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:27

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesemea Uchumi wa Buluu ni dhana inayochagiza...

BARRICK NI KIELELEZO BORA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI NCHINI- DKT. KIRUSWA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:20

 • Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...

WAKURUGENZI WA UFUATILIAJI NA TATHMINI NGAZI YA WIZARA WAKUTANA KUPITIA TAARIFA YA UTENDAJI WA SERIKALI

msumbanews.co.tz - 12/Feb 15:36

 Na Mwandishi wetu - Iringa.Wakurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini ngazi ya wizara wamekutana leo tarehe 12 Februari 2025 katika Ukumbi wa Mkuu wa...

RAIS SAMIA AKABIDHI BOTI 35 KWA WAVUVI TANGA

msumbanews.co.tz - 09:01

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Februari 26, 2025 amekabidhi boti 35 za kisasa kwa...

MAKAMU WA RAIS ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA VIPINDI VYA ELIMU KWA UMMA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:32

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...

RAIS SAMIA KUZINDUA DARAJA LA PANGANI NA BOTI ZA UVUVI.

msumbanews.co.tz - 04:16

 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo anaendelea na ziara yake mkoani Tanga ambapo pamoja na mambo mengine,...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément