Na Josephine Maxime- Dar es Salaam Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko ameagiza Mwanafunzi Mirabelle...
Vous n'êtes pas connecté
📌 Asema mradi umefikia asilimia 99.8📌 Awaasa watanzania kujivunia mradi wa Julius NyerereKatibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameipongeza Wizara ya Nishati kwa usimamizi wa mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere utakaozalisha Mw 2115 na hivyo kuleta ziada ya upatikanaji wa Umeme hapa nchini.Msigwa ametoa pongezi hizo leo Februari 16, 2025 katika eneo la mradi wa Julius Nyerere katika Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari wenye lengo la kuzungumzia mafanikio kwenye sekta ya nishati sambamba na maendeleo ya mradi wa kufua Umeme wa JNHPP."Wizara hii kupitia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Mhe. Dkt Doto Biteko,inafanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi huu na mingine ambayo inawanufaisha watanzania kwa kuwapatia umeme wa kutosha." Amesema Msigwa.Amesema mradi wa bwawa la Julius Nyerere unahusisha mambo makubwa matatu ambayo ni upatikanaji wa umeme, kilimo kwenye umwagiliaji pamoja na uvuvi kwenye ufugaji na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwa maslahi mapana ya nchi.Aidha, mradi ulianza kujengwa mwaka 2019 kwa gharama ya shilingi trillioni 6.558 ambapo hadi sasa umefikia asilimia 99.8 na mashine nane Kati ya Tisa zimesha kamilika ambazo zimeingiza kwenye gridi ya Taifa megawati kwa jumla ya megawati 1,880.Msigwa amesisitiza kuwa mashine ya mwisho namba tisa utekelezaji wake umefika asilimia 98 huku majaribio ya mtambo huo yakitarajiwa kuanza majaribio Februari 25 na Machi 10 utaingiza umeme kwenye gridi ya Taifa ili kukamilisha megawati 2,115.Katika hatua nyingine ametoa rai kwa Watanzania kujivunia mradi wa Julius Nyerere kutokana na ukubwa wake si katika bara la Afrika peke yake na Dunia kwa ujumla.
Na Josephine Maxime- Dar es Salaam Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko ameagiza Mwanafunzi Mirabelle...
• Tanzania, Rwanda na Uganda zakubaliana kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Kufua Umeme Nsongezi wa 39MWMkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri...
📌 Tanzania, Rwanda, Uganga kusaini MOU kuendeleza mradi wa kufua umeme wa pamoja wa Nsongezi📌 Baraza kusimamia Kongamano na Maonesho ya 11...
Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga.Moja ya changamoto kubwa inayoikabili dunia kwa sasa na Tanzania ikiwepo ni tatizo la ajira hasa kwa vijana. Nchini...
Na Denis Chambi , Tanga.SERIKALI imeanza mchakato wa uboreshaji wa miundombinu ya Bomba la Tazama linalosafirisha mafuta kutoka Tanzania hadi...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bitekoakizungumza na Watanzania waishio India pamoja na watumishi wa Ubaloziwa Tanzania...
Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido akitoa taarifa ya utendaji wa Barrick na Twiga kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na...
• Yachangia Zaidi ya Shilingi Trilioni 11 katika Uchumi wa Tanzania• Gawio la Zaidi ya Shilingi Bilioni 412 latolewa kwa SerikaliKampuni ya...
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimesaini mkataba na kampuni ya kandarasi ya Arm-Strong International Ltd ya jijini Mwanza kuanza ujenzi wa...