X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 11/Sep 06:30

HAKI ELIMU : VIJANA WENGI WA SEKONDARI HAWANA UELEWA NA DEMOKRASIA

Mkuu wa Idara ya Utafiti kutoka Haki Elimu Makumba Mwemezi amesema utafiti uliofanywa na Taasisi hiyo umebaini kuwa asilimia 44.4 ya vijana katika shule za sekondari nchini hawana uelewa wa mambo gani yanayounda demokrasia huku asilimia 3.8 hawajui chochote kuhusu demokrasia."Kupitia utafiti huu tumegundua kuwa nchini Tanzania, elimu ya uraia ni sehemu ya mtaala wa shule, ambayo inalenga kuandaa wanafunzi wenye ufaulu wa juu kuliko kuwafundisha mchakato wa demokrasia" amesema Mwemezi na kuongeza"Hata hivyo kuna wasiwasi mkubwa wa kupungua kwa vijana wanaoshiriki mchakato wa demokrasia kwani asilimia 29 ya wanafunzi wanakiri kuwa viongozi wa wanafunzi wanapatikana kwa kuteuliwa na walimu"Mwenezi amesema Haki Elimu imeendesha programu ya Kivunge cha elimu ya uraia kwa shule za secondari kinacholenga kulea na kukuza ushiriki wa vijana Katika shughuli mbalimbali za kidemokrasia kuanzia darasani, shuleni hadi kwenye jamii.Akichangia mada Katika mdahalo huo, mtoa mada Arif Fazel ambaye pia ni meneja mradi wa Action Aid amewataka vijana wenye nafasi ya kuwafikia vijana wenzao kufanya hivyo ili kuhakikisha kila kijana anakuwa sehemu ya utekelezaji wa maamuzi aliyoyapitisha."Mimi binafsi nimeshiriki katika michakato mbalimbali ya kidemokrasia, na hii inatokana na nafasi niliyonayo, sasa je ni vijana wangapi ambao wana nafasi kama yangu? Hivyo sisi wenye nafasi tutumie rasilimali ndogo tulizonazo kuhakikisha na wenzatu wanafikiwa? Alisema FazelTumsume Vibweja kutoka Mbeya anasema vijana hawashirikishwi vya kutosha Katika michakato ya demokrasia akitolea mfano mchakato unaendelea wa kutoa maoni kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Taifa 2050."Sisi vijana hasa wa vijijini bado hatushirikishwi inavyotakiwa zaidi tunaletewa taarifa ambazo zimeshapitishwa, mfano halisi ni hili zoezi ya Dira ya Taifa, binafsi nimefanya jitihada kubwa sana kushiriki lakini licha ya kupata nafasi ya kushiriki lakini sikupata nafasi ya kutoa mawazo yangu" alisema Vibweja.

Articles similaires

WIKI YA AZAKI KUHAMASISHA JAMII KUSHIRIKI DIRA 2050, UCHAGUZI

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:02

 Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society FCS- Justice Rutenge, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini...

DC Mpogolo aendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Ukonga

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:47

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga...

WANAWAKE LONGIDO WAJENGEWA UWEZO KUTAMBUA HAKI ZAO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 06:22

 Wanawake kutoka jamii ya kimaasai katika Tarafa ya Longido wilaya ya Longido mkoa wa Arusha wameonyesha furaha yao baada ya shirika la Legal...

NG'UMBI AWATAKA WADAU KUONGEZA USHIRIKIANO KATIKA ELIMU

msumbanews.co.tz - 16:38

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Michael Ng’umbi akifafanua jambo wakati wa mahojiano maalum kuhusu hali ya elimu nchini kupitia...

Kamati ya Bunge Yaipongeza UDSM kwa Maboresho ya Mitaala na Utekelezaji wa Mradi wa HEET

msumbanews.co.tz - 11/Sep 04:51

 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi...

WAZIRI JAFO ATAKA WANANCHI KUACHA KUCHANGANYA MAZAO

msumbanews.co.tz - 10:06

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakitembelea na kukagua Ghala la Mpako...

SHULE 26 ZAJENGWA NCHINI KUONGEZA MKAZO MASOMO YA SAYANSI KWA WASICHANA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 11:21

Serikali imeongeza mkazo katika masomo ya Sayansi ikiwa ni pamoja na kujenga shule 26 za wasichana zinazotoa masomo ya Sayansi.Hayo yamesemwa na...

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO ATOA WITO WA MABORESHO KATIKA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 05:59

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma...

WANANCHI LONGIDO WATAKA SHULE ZA BWENI KUIMARISHWA ULINZI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:12

Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wameiomba serikali kujengea uzio shule zote za serikali za bweni zilizopo katika wilaya hiyo lengo ni...

DODOMA, MANYARA NA SINGIDA KUANZA UBORESHAJI SEPTEMBA 25,2024 - INEC

msumbanews.co.tz - 13/Sep 13:04

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji Mstaafu Mahakama ya Rufaa Mbarouk Salim Mbarouk ,akizungumza leo Septemba 13,2024...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément