Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); tarehe 24 Oktoba 2024 imemtambulisha rasmi mkandarasi; kampuni ya CCC (Beijing) Industrial &...
Vous n'êtes pas connecté
MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Umeme kwenye vitongoji 135 Mkoani humo katika majimbo yote tisa.Ametoa pongezi hizo leo Septemba 12, 2024 ofisini kwake wakati akizungumza na Ujumbe wa wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliomtembelea wakiongozana na Cylex Engineering Company ambaye ndie mkandarasi wa mradi.Amesema Mhe. Rais anaendelea kuboresha maisha ya wananchi wake kwa kasi ndio maana amemaliza kuweka huduma za umeme kwenye vijiji vyote nchini na sasa anaelekeza nguvu kwenye vitongoji kwa kuhakikisha wanapata Nishati Safi.Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa Wakala kumsimamia Mkandarasi vema ili akamilishe mradi kwa wakati kwa mujibu wa mkataba ili kwa haraka huduma za umeme ziweze kuwafikia wananchi.Vilevile, amemtaka mkandarasi huyo kutumia wananchi wazawa kwenye maeneo ya mradi katika ajira ndogondogo zitakazotolewa na kuhakikisha wanawalipa kwa wakati ili kuepusha migogoro isiyo lazima kwenye eneo la kazi.Akizungumzia upatikanaji wa huduma ya umeme Mhe. Mtanda amesema Mwanza ina nishati ya kutosha kwani ni megawati 86 pekee zinatumika kwa sasa pamoja na kuzalishwa zaidi ya megawati 100 hivyo kumekua na ziada ambayo itatumika pindi miradi ya kimkakati itakapoanza.Awali, Msimamizi wa miradi ya Wakala wa Nishati vijijini REA Kanda ya ziwa Mhandisi Ernest Makale amesema mradi huo kwenye vitongoji unadhihirisha na kubainisha nia ya serikali ya kuhakikisha kila kitongoji nchini kinakua na umeme ifikapo 2030.
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); tarehe 24 Oktoba 2024 imemtambulisha rasmi mkandarasi; kampuni ya CCC (Beijing) Industrial &...
Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi wa kuiunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na umeme wa gridi kutokea...
-AISISITIZA KUENDELEA NA UHAMASISHAJI-REA YAELEZEA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINIWaziri wa Maji,...
Kuhusisha transfoma za kVA50, 100 na 200Vitongoji ambavyo havijapata umeme kufikiwaNaibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali...
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa wito kwa Wabunifu na Wakadiriaji majenzi nchini kuwa Wazalendo, Waadilifu na Wabunifu kwa Taifa katika...