Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakary Zubeiry bin Ally, amempongeza Dkt. Shehnaz Shaikh kwa kazi yake ya kujitolea katika kuandaa tafsiri...
Vous n'êtes pas connecté
LSF nao kuendelea kusaidia vikundi wanawake Longido.Shirika la Wanahabari la usaidizi wa.jamii za pembezoni(MAIPAC) linatajia kuzindua mradi kabambe wa kuelimisha juu ya athari za ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa kutetea haki zao.Mradi huo unafadhiliwa na shirika la Cultural Survival na unatarajiwa kusaidia pia kupaza sauti za vijana wanaopinga vitendo vya ukeketaji.Mkurugenzi wa Shirika la MAIPAC Mussa Juma alitoa taarifa hiyo katika ziara iliyofanywa na Asasi za kirai katika wiki ya Asasi hizo iliyofanyika wilayani Longido ."MAIPAC imebaini kuwa watoto wa miaka miwili hukeketwa katika Jamii ya Kimasai hivyo tunampango wa kuzindua mradi wa kuelemisha kuhusu masuala mazima ya ukeketaji na ukatili kwa watoto wa kike , lakini pia kuwajengea Uwezo wa kujiamini wanawake wa kimasai na kuweza kutetea haki zao za msingi hasa katika kukemea Ukatili" amesema.Katika Ziara iliyofanywa na Asasi za kiraia (CSO) wadau wa asasi hizo wamepata wasaa wakutembelea kikundi cha wanawake wanaofadhiliwa na shirika la Legal Service Facility(LSF) na Vodacom Foundation.Akizungumza na ziara hiyo mkurugenzi wa LSF ,Lulu Ng'wanakilala alisema shirika hilo limekuwa likisaidia vikundi 11 vya wanawake wa jamii ya kifugaji kata Kimokoa wilaya ya Longido.Ng'wanakilala alisema wanawake wa jamii za kifugaji bado wanakaniliwa na changamoto ikiwepo changamoto za kiuchumi,ushiriki katika siasa na changamoto za kiafya.Hata hivyo alisema kupitia mradi wanaotekeleza longido wameweza kusaidia jamii ya wanawake kiuchumi kwa kuwa na miradi midogo,ushiriki katika masuala ya kisiasa na kupambana na changamoto za kiafya ikiwepo ikeketaji.Katika wiki ya CSO hufanyika mara moja kila mwaka ambapo zaidi ya Wadau 600 wameweza kushiriki na kushirikishana Masuala mbalimbali ya kijamii kwa njia ya midahalo na Majadiliano ya kina yanayolenga Mchango wa CSOs hizo kwa maendeleo ya Taifa.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakary Zubeiry bin Ally, amempongeza Dkt. Shehnaz Shaikh kwa kazi yake ya kujitolea katika kuandaa tafsiri...
SHIRIKA la Grumeti Fund kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii limejivunia mafanikio yake katika kutoa elimu ya kijinsia kwa vijana wa kike na wa kiume...
Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...
Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba madelu (Mb), akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika...
Na;Jusline Marco :ArushaWaziri wa Afya nchini Jenista Mhagama amewataka wadau wa afya kuendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha utoaji wa...
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji ...
Na. Scola Malinga, WF, Dar es SalaamNaibu waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa kuandaa...
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, amewahimiza wananchi wa wilaya hiyo kujikita zaidi katika lishe bora na kuachana na tabia ya ulaji usiofaa...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameliomba Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na...