X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 01/Nov 08:25

CHANDE ASHAURI MABENKI KUTANUA WIGO WA MASOKO NJE YA NCHI

 Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB) kuendelea na jitihada za kuongeza wigo wa uwekezaji na masoko nje ya nchi ili kujiimarisha.  Mhe. Chande ametoa rai hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc (ACB), Bw. Silvest Arumasi, kuhusu fursa za maendeleo, Ofisini kwake, jijini Dodoma. Alisema kuwa Sekta ya Benki nchini ikikua, itatoa fursa kwa Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia benki za ndani kuliko kulazimika kwenda kutafuta fedha kwenye benki za nje ambazo hazimnufaishi mwananchi kwa kiwango kikubwa. “Lengo la Serikali ni kuhakikisha inakuza sekta ya Benki hususani Benki za Ndani ili kuchochea maendeleo”, alisema Mhe. Chande. Aidha, ameihakikishia Benki hiyo kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nayo pamoja na Benki nyingine nchini kwa kuwa lengo la Serikali kupitia Wizara ya Fedha ni kuhakikisha sekta ya Benki inaimarika na kutoa mchango katika maendeleo ya nchi. Alisema Tanzania imeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya kibenki katika Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yamekuwa na mchango katika maendeleo ya sekta mbalimbali. Ameipongeza Benki ya ACB kwa kuendelea kufanya jitihada za kujimarisha ili kutoa huduma bora kwa wateja wake na Tanzania kwa ujumla. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc (ACB), Bw. Silvest Arumasi, aliipongeza Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara na akaahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwahudumia wananchi. Alisema kuwa Benki hiyo imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuwahudumia wajasiriamali wadogo lakini inaendelea na jitihada za kuwafikia watu wengi zaidi.

Articles similaires

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

msumbanews.co.tz - 13:07

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...

TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

msumbanews.co.tz - 13:07

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...

SERIKALI KUHAKIKI WASTAAFU KIDIJITALI

msumbanews.co.tz - 08/Nov 11:56

Na: Farida Ramadhan na Josephine Majura WF, DodomaSerikali inatengeneza mfumo wa kidigitali utakaowawezesha Wastaafu kujihakiki wenyewe (Self...

Jakaya Kikwete aipongeza NMB kwa Bil. 1 za Matibabu ya Watoto JKCI

msumbanews.co.tz - 04/Nov 08:09

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, amekiri kuvutiwa na mchango mkubwa wa Benki ya NMB wa Sh. Bilioni 1 kati ya Sh. Bil....

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

AICC NI MUHIMILI WA SEKTA YA UTALII NCHINI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:36

 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément