X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 05/Nov 17:14

SERIKALI YAFAFANUA MSAMAHA WA KODI KWENYE VYAKULA VYA MIFUGO

 Na. Asia Singano na Peter Haule, WF, Dodoma.Serikali imesema kuwa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani imetoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye uingizwaji wa vyakula vya mifugo ikiwemo vyakula vya Samaki vinavyotambulika kwa HS Code 23.09 chini ya utaratibu wa utozaji ushuru wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupunguza kodi ya uingizaji wa vyakula vya samaki nchini.‘’Vifaa vinavyoagizwa kutoka nje na watu wanaojihusisha na ufugaji wa samaki na kilimo ambavyo Kamishna ameridhika kuwa ni kwa matumizi katika sekta ya ufugaji wa samaki vimeondolewa Ushuru wa Forodha kwa mujibu wa Kifungu cha 15(a) cha Sehemu B ya Jedwali la Tano ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, alisema Mhe. Nchemba.Dkt. Nchemba alifafanua kuwa Serikali inaendela kuongea na sekta ili kuona maeneo ambayo yanastahili kupata ruzuku na tayari baadhi ya maeneo Serikali inatoa ruzuku na itaendelea kutoa ruzuku katika maeneo mbalimbali kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha.Aliongeza kuwa Serikali inaweka vivutio kwenye uzalishaji wa bidhaa ili kujitosheleza ndani ya nchi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje na kuwa itaangalia maeneo ya maboresho katika bajeti ijayo kufanikisha kuongeza uzalishaji wa ndani.

Articles similaires

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

WAZIRI JENISTA ASISITIZA ULAJI WA LISHE BORA YENYE KUZINGATIA VIRUTUBISHI

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:39

 Na;Jusline Marco :ArushaWaziri wa Afya nchini Jenista Mhagama amewataka wadau wa afya kuendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha utoaji wa...

ZAIDI YA WANANCHI 32,000 WA VIJIJI VYA WILAYA ZA MOROGORO NA MVOMERO KUANZA KUPATA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 18:47

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:22

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA WADAU KUJIKITA VIJIJINI, ELIMU YA KUPINGA UKATILI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:24

  Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA UTAIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA KIGOMA- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:10

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément