Na Munir Shemweta, WANMM Bukoba Tanzania na Uganda zimetia saini makubaliano ya uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo...
Vous n'êtes pas connecté
Na Munir Shemweta, WANMM Bukoba Kikao cha Kamati ya Pamoja cha Wataalamu wa Tanzania na Uganda (JTC) kimeanza mkoani Kagera nchini Tanzania kujadili uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo. Kikao hicho kimeanza tarehe 5 Novemba 2024 na kutarajiwa kumalizika Novemba 7, 2024 kinafanyika katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kuhusisha wataalamu kutoka nchi za Tanzania na Uganda. Akifungua kikao hicho cha siku tatu kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Abuubakar Mwasa, katibu Tawala mkoa wa Kagera Bw. Stephen Ndaki amesema, Tanzania imejipanga kikamilifu kutekeleza zoezi la uimarishaji mpaka wa kimataifa kwa ajili ya ustawi wa nchi hizo mbili. Amebainisha kuwa, uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Uganda una lengo la kuweka usimamizi mzuri wa mpaka baina ya nchi hizo pamoja na kukuza amani, upendo, usalama na maisha ya watu wake. Kupitia hotuba hiyo ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, Bw. Ndaki amesema, Tanzania na Uganda zimekuwa na mahusiano mazuri ikiwemo tamaduni zinazofanana alizozieleza kuwa, zimewezesha wananchi wa nchi hizo mbili kuishi kwa upendo. "Ni imani yangu kila mshiriki katika kikao hiki atatumia muda kuhakikisha uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi zetu unakuwa na matokeo mazuri kwa ustawi wa nchi na wananchi wetu" amesema. Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni mkuu wa timu ya Tanzania katika kikao hicho Bw. Hamdouny Mansoor amesema, mkutano huo ni utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika kuhusu uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa nchi za Afrika kufikia mwaka 2027. "Ni nia ya Umoja wa Afrika kuzifanya nchi za Afrika kuwa na amani pasipo migongano wakati wa zoezi zima za uimarishaji mipaka ya kimataifa" amesema Mansoor. Kwa upande wake Mkuu wa ujumbe wa timu ya wataalamu kutoka Uganda Bi. Jacqueline Banana Wabyona ameihakikishia Tanzania ushiriki mzuri kwenye kikao hicho kwa lengo la kufikia matokeo chanya ya uimarishaji mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Mpaka wa Tanzania na Uganda una urefu wa takriban km 397.8 ambapo kati ya hizo km109 ni nchi kavu , km 42.8 ni sehemu ya mto kagera na km 246 ni sehemu ya ziwa victoria. Zoezi la uimarishaji mipaka ya kimataifa ni utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Afrika kuwa, ifikapo mwaka 2027 mipaka baina ya nchi za Afrika iwe imeimarishwa. Tanzania imepakana na nchi 10 ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, DRC, Zambia, Malawi, Msumbiji, Comoro na Shelisheli huku mipaka baina ya nchi hizo ikiwa imegawanyika katika sehemu mbili za nchi kavu na majini.
Na Munir Shemweta, WANMM Bukoba Tanzania na Uganda zimetia saini makubaliano ya uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo...
Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...
Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...
Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...
Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam 04/11/2024 Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Watu wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ameziomba Taasisi ya...
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa wito kwa Wabunifu na Wakadiriaji majenzi nchini kuwa Wazalendo, Waadilifu na Wabunifu kwa Taifa katika...