X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 18/Sep 07:03

MAGARI YENYE MFUMO MBOVU WA BREKI YAKAMATWA MKOANI SONGWE

Wamiliki wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kuhakikisha Madereva wa vyombo hivyo wanafuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja tabia ya kuendesha magari ya abiria na mizigo bila kukagua magari wanayoyaendesha ili kubaini mapungufu yaliyonayo.Kauli hiyo imetolewa Septemba 17, 2024 na Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassor Sisiwaya alipokuwa kituo cha ukaguzi wa Magari Chimbuya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe kwenye operesheni maalumu za ukaguzi zinazoendelea nchini kote.Vilevile, ACP Sisiwaya amewataka madereva kukagua magari yao kabla ya kuanza safari pia aliwataka wamiliki wote wa vyombo hivyo vya moto kuhakikisha magari yao yanakaguliwa na kupata stika ya NENDA KWA USALAMA.Naye, Kaimu Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani humo, Mkaguzi wa Polisi Fidelia Kasongwa amesema kuwa, Jeshi la Polisi limebaini na kuyakamata magari ya mizigo na abiria 07 ambayo mifumo yake ya breki haipo sawa na kupelekea madhara kwa abiria na chombo kutokana na mazingira ya Mkoa wa Songwe kuwa na milima, miteremko na kona nyingi ambapo gari lisipokuwa na breki linaweza kuleta madhara kwa dereva, abiria na watumiaji wengine wa barabara.Aidha, Mkaguzi wa Magari wa Polisi Mkoa wa Songwe Koplo Samwel Mtatiro amewakumbusha wamiliki wote wa magari kuwakumbusha mara kwa mara madereva wao kuwa makini na kufuata sheria za usalama barabarani pindi wawapo safarini na kufichua utovu wa nidhamu unaofanywa na baadhi ya madereva wengine ambao unahatarisha usalama kwa watumiaji wengine wa barabara ambapo amewataka watumiaji wote wa vyombo vya moto kuhakikisha vyombo hivyo vinakuwa salama wakati wote.Kwa upande wake dereva mmoja wapo aliyekamatwa kwa kosa la mfumo wa breki amesema kuwa tatizo hilo linatokana na ubovu wa barabara za nchi jirani ambazo zinapelekea matairi kuisha na kupata tatizo la kufeli breki na kuwaomba matajiri wa magari hayo kuweza kuyatengeneza ili kuwa salama kwenye safari zao wakati wote kwa lengo la kuepusha madhara kwenye jamii na miundombinu ya barabara.

Articles similaires

MAGARI YENYE MFUMO MBOVU WA BREKI YAKAMATWA MKOANI SONGWE

msumbanews.co.tz - 18/Sep 07:03

Wamiliki wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kuhakikisha Madereva wa vyombo hivyo wanafuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja tabia ya...

TANAPA yaanza na mkakati wa kuboresha barabara zilizopo Hifadhi za Taifa hususani barabara ya Serengeti

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:02

 WADAU wa Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wameiomba Serikali kupatia suluhisho la kudumu la ujenzi wa barabara katika Hifadhi za Taifa...

VIJANA WA BODABODA 180 WA BUKOBA MJINI WALIPIWA MAFUNZO YA UDEREVA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 09:30

Shirika la Omuka Hub lililo chini ya Mhe Neema Lugangira ambae  ni Mlezi wa Chama cha Madereva wa Pikipiki na Wamiliki  Bukoba Mjiniwamezindua Kozi...

KUUZA NA KUHIFADHI MAFUTA YA PETROLI KWENYE MADUMU,CHUPA NI HATARI KWA AFYA,MAZINGIRA

msumbanews.co.tz - 16/Sep 11:14

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewaagiza wamiliki wote wa vituo vya mafuta ya petroli nchini kuhakikisha wanachukua hatua...

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO ATOA WITO WA MABORESHO KATIKA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 05:59

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma...

BoT, AZAKI WAJADILI KUBORESHA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA KWA JAMII

msumbanews.co.tz - 08:23

 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema itaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kusaidia ukuaji wa huduma za malipo kidigitali kwa kuweka miundombinu...

POLISI WAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CHADEMA ,CCM WALAANI UTEKAJI

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:02

Jeshi la polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama cha upinzani Chadema kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe...

TANZANIA YAWEKEZA KIMKAKATI KATIKA SEKTA YA TEHAMA ILI KUKUZA UCHUMI WA KIDIJITALI

msumbanews.co.tz - 08:01

Tanzania ina mifumo kadhaa ya kisheria na udhibiti inayoongoza sekta ya mawasiliano na TEHAMA ili kuhakikisha huduma ya intaneti ya kasi inawafikia...

NI MARUFUKU BIASHARA YEYOTE YA MADINI KUFANYIKA MAJUMBANI WILAYANI TUNDURU – WAZIRI MAVUNDE

msumbanews.co.tz - 17/Sep 16:46

 Waziri wa Madini Anthony Mavunde amepiga marufuku biashara ya madini kufanyika majumbani kwa watu na kusisitiza kwamba hatua kali za kisheria...

KISHINDO CHA TAMASHA LA UTAMADUNI RUVUMA,RAIS SAMIA APONGEZWA

msumbanews.co.tz - 14/Sep 11:05

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ahmed Abbas Ahmed ,akizungumza na wamiliki wa hoteli kuhusu fursa za Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Baadhi ya wamiliki wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément