Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...
Vous n'êtes pas connecté
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua rasmi zahanati ya Ivilikinge iliyopo Wilayani Makete Mkoani Njombe sambamba na kukabidhi vifaa mbalimbali vya hospitali vilivyotolewa na Benki ya NMB.Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, leo Septemba 16,2024, Mhe. Chana amesema uwepo wa zahanati hiyo ni miongoni mwa vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan vya kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi mpaka vijijini." Hizi ni baadhi ya huduma tulizoahidi kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo tunapochagua viongozi tuchague ambao watatuletea maendeleo" amesisitiza Mhe. Chana.Amesema kuwa kupitia zahanati hiyo wananchi wa Isapulano na vijiji vya jirani watapata huduma bora za afya na kuwaomba wananchi hao kuhakikisha wanaitumia ipasavyo zahanati hiyo.Naye, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Willy Mponzi amesema kwa kuzingatia juhudi za Rais katika kusimamia upatikanaji wa huduma bora za afya mijni na vijijini, changamoto za Sekta ya Afya ni kipaumbele kwa Benki ya NMB kwa sababu afya ni kipaumbele kwa maendeleo ya Taifa lolote.Kufuatia hatua hiyo,benki ya NMB inakabidhi vifaa mbalimbali vya hospitali kwa zahanati hiyo ikiwemo Vitanda vya kujifungulia (2),Vitanda vya uchunguzi (2),vitanda vya hospitali (5),Magodoro (5),folding screen (4),folding stretcher (2),delivery kit (5),drip stend(5), mashuka 50 na viti vyenye magurudumu (3) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9.Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Isapulano, Hassan Omar alisema kuwa mradi huo umegharimu takribani milioni 146.1 ambayo inatokana na michango ya wananchi (milioni 26.5), Wadau wazawa (milioni 6.6, Mbunge wa Jimbo la Makete,Mhe. Festo Sanga (milioni 4) ,Diwani (laki 5 na elfu 30), Benki ya NMB Mabati (milioni 8.5) na Serikali (milioni 100).Amefafanua kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Ivilikinge na vijiji vya jirani, kupunguza umbali wa kufuata huduma kwa mama wajawazito, watoto na wazee.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...
Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam 04/11/2024 Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Watu wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ameziomba Taasisi ya...
Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kujenga nyumba zenye uhitaji katika...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea...
Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba madelu (Mb), akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika...
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...