X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 28/Oct 12:48

KC Kitunda Yaimarisha ushiriki wa wanawake kwenye maamuzi

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMKITUO Cha Taarifa na Maarifa katika kata ya Kitunda kimefanikiwa kuibua ajenda za kijamii na kuhamasisha usalama wa watoto wa kike pamoja na ushiriki wa wanawake katika uongozi, kufuatia kufanya tathimini ya mradi wa Women’s Leadership and Economic Rights (WLER).Kituo hicho kimewezesha jamii kukubaliana na mpango wa kujenga uzio katika shule zote za kata hiyo ili kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mazingira hatarishi, sambamba na kuwawezesha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uamuzi na uongozi.Akizungumza katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kituo hicho, Bi. Claudia Gabriel Kawonga, amesema mradi huo umeleta mabadiliko ya kimtazamo katika jamii, hasa katika kuthamini mchango wa wanawake.“Baada ya kufanya tathimini ya mradi, tulipeleka mrejesho serikalini na kuanzisha mpango kazi tuliojiwekea. Tulizungumza na walimu, wazazi na viongozi wa mitaa, na wote tumekubaliana kwamba shule zetu ziwe na uzio ili kulinda watoto wetu,” amesema.Bi. Claudia ameongeza kuwa kabla ya mradi huo, wanawake wengi walikuwa na hofu na dhana potofu kuhusu uongozi, lakini baada ya mafunzo na hamasa, baadhi yao wamepata nafasi za uwakilishi katika serikali za mitaa.Kwa upande wake, Mwanaharakati wa masuala ya kijinsia wa kata hiyo, Bi. Mwajuma Kidulazi, amesema mradi wa WLER pia umechochea ufuatiliaji wa ajenda nyingine za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara na uanzishwaji wa soko la kisasa katika kata hiyo.“Barabara tayari tumeanza kuona utekelezaji kupitia serikali. Kuhusu soko, tumekubaliana baada ya uchaguzi kukamilika tukutane na mbunge atakayechaguliwa ili kuwasilisha rasmi changamoto hiyo,” amesema.Licha ya hatua chanya zinazofikiwa nchini ikiwemo historia ya Tanzania kumpata Rais mwanamke kwa mara ya kwanza, wanawake wengi bado wanakabiliwa na changamoto zinazotokana na mfumo dume, umaskini na ubaguzi wa kijinsia.Mradi wa WLER umeendelea kujikita katika kuhamasisha usawa wa kijinsia, kuwajengea wanawake ujasiri wa kushiriki katika maamuzi, na kubadilisha mitazamo inayowanyima fursa.

Articles similaires

KC Kitunda Yaimarisha ushiriki wa wanawake kwenye maamuzi

msumbanews.co.tz - 28/Oct 12:48

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMKITUO Cha Taarifa na Maarifa katika kata ya Kitunda kimefanikiwa kuibua ajenda za kijamii na kuhamasisha usalama wa...

MRADI WA WLER WALETA MAPINDUZI MAKUBWA YA USAWA WA KIJINSIA CHANIKA

msumbanews.co.tz - 25/Oct 18:36

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMKituo cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Chanika kimeibuka na ajenda ya kuimarisha miundombinu ya shule na uwezo wa...

MRADI WA WLER WAIBUA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU GONGO LA MBOTO

msumbanews.co.tz - 25/Oct 20:10

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAMWANAWAKE wa Kata ya Gongo la Mboto wamehamasishwa kushiriki katika nafasi za uongozi na kujiimarisha kiuchumi...

KUKAMILIKA KWA MRADI WA AGRI-CONNECT UTABADILI TASWIRA YA MIUNDOMBINU MBINGA

msumbanews.co.tz - 27/Oct 12:40

 Katika juhudi za kuboresha miundombinu na kuinua uchumi wa wakazi wa wilaya ya Mbinga, Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)...

KUKAMILIKA KWA MRADI WA AGRI-CONNECT UTABADILI TASWIRA YA MIUNDOMBINU MBINGA

msumbanews.co.tz - 27/Oct 12:40

 Katika juhudi za kuboresha miundombinu na kuinua uchumi wa wakazi wa wilaya ya Mbinga, Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)...

NAMELOK ATOA SOMO NAMNA YA UPIGAJI KURA KWA JAMII YA KIFUGAJI YA KIMASAI

msumbanews.co.tz - 28/Oct 19:06

MJUMBE wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Namelok Sokoine Ametoa somo la elimu ya jinsi ya kupiga kura kwa jamii ya...

NAMELOK ATOA SOMO NAMNA YA UPIGAJI KURA KWA JAMII YA KIFUGAJI YA KIMASAI

msumbanews.co.tz - 28/Oct 19:06

MJUMBE wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Namelok Sokoine Ametoa somo la elimu ya jinsi ya kupiga kura kwa jamii ya...

WAKUU WA VITENGO VYA UFUATILIAJI NA TATHMINI WA SEKRETARIETI ZA MIKOA WAJENGEWA UWEZO WA MASUALA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI NCHINI

msumbanews.co.tz - 23/Oct 17:22

 Na Mwandishi WETU, SINGIDAOfisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeandaa kikao kazi cha siku 3 kilichowakutanisha Wakuu   vitengo vya...

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU KUJENGA KAMPASI MPYA MAKAMBAKO

msumbanews.co.tz - 22/Oct 09:54

 Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Fatma Mode wamefanya ziara ya...

DKT. MATARAGIO AAGIZA VIFAA VYOTE VYA UHAKIKI WA JOTOARDHI ZIWA NGOZI KUFIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 22/Oct 17:36

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni yake Tanzu ya Uendelezaji...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément