Na Dk. Reubeni LumbagalaChama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kikongwe nchini, sasa kimetimiza miaka 48 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977. Ukongwe wa...
Vous n'êtes pas connecté
NNaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara (UVCCM), Mussa Mwakitinya amesema ushindi kwa Chama cha Mapinduzi sio ombi bali ni lazima kutokana na kazi kubwa zilizofanyika chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo zinauzika kwa wananchi. Aidha alisema kuwa lengo la Chama hicho kuendelea kushika dola sio kwenda kucheza rede bali ni kuendelea kutatua shida na changamoto za wananchi. Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec) alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa kambi ya Vijana wa ccm mkoa wa Kilimanjaro wapatao zaidi ya 700 inayofanyika wilayani Hai. Alisema kuwa, hakuna Chama cha siasa kinachoweza kutatua matatizo ya Wananchi katika Taifa hili zaidi ya Chama cha Mapinduzi na kuwataka wananchi kutodanganyika na watu wenye nia hovu na Taifa. "Vijana mnapaswa kutambua kuwa CCM sio Chama ambacho kinatafuta dola ili kwenda kucheza rede bali ni kuendelea kutatua matatizo ya wananchi na ndio maana mmeshuhudia fedha nyingi zimetolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo" Alisema Mwakitinya. Aliwataka Vijana kusimamia maadili na kuchunga njia zao kama vijana wa CCM ili kuendelea kuwavutia vijana walio nje ya Chama kujiunga na Chama hicho. Alisema kuwa, CCM kinamisingi ya Umoja na mshikamano na kuwataka kutokuruhusu kutengana kwani itaruhusu kuingiliwa na maadui na kuruhusu Chama kushindwa katika chaguzi mbalimbali. "Ili Chama kiendelee kuwa imara ni lazima kushikamana hivyo vijana mnawajibu wa kutambua kuwa Chama kinawahitaji katika kuhakikisha wagombea wake wanashinda hivyo tuendelee kuilinda na kuitunza imani hiyo tuliyopewa na Chama chetu" Alisema Mwakitinya. Akitoa taarifa ya kambi hiyo, Katibu wa UVCCM mkoa Kilimanjaro, Ahmady Kibamba alisema kuwa, vijana wameamua kujinoa, kujiivisha na kujiimarisha ili kuweza kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kibamba alisema kuwa, kambi hiyo itaanza Februari 25 mwaka huu hadi Machi 2 ambapo vijana zaidi ya 700 kutoka wilaya saba za mkoa wa Kilimanjaro wameshiriki katika kambi hiyo. Kwa upande wake, Mbunge wa viti maalum kupitia Vijana, Asia Halamga alisema kuwa, kijana aliyepo ndani ya Chama cha Mapinduzi anakuwa katika njia sahihi na kuwataka vijana kuendelea kujiunga na Chama hicho. Asia alisema kuwa, vijana wa Kilimanjaro hawajawahi kurudi nyuma hasa linapokuja swala la Uchaguzi na kudai kuwa katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu watahakikisha Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Wabunge na Madiwani watakaopeperusha bendera ya CCM wanapata kura nyingi na za kishindo.
Na Dk. Reubeni LumbagalaChama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kikongwe nchini, sasa kimetimiza miaka 48 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977. Ukongwe wa...
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi (CCM)...
Na Oscar Assenga, TANGAMABALOZI 23 wa Mkoa wa Tanga unaoundwa na Wasanii wa Filamu,Waandishi pamoja na watangazaji wametua Jijini Tanga kwa lengo la...
Katibu tawala wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele akimkabidhi Tuzo ya Walipakodi Bora kwa Wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha...
Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old ShinyangaWajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika...
Wadaia kugawa hongo kati ya Sh.5000 na Sh.50,000 ,Mbunge mwenyewe atoa majibuNa Shomari Binda,RoryaWAKATI joto la uchaguzi ndani ya Chama Cha...
▪️Asisitiza Rais Dkt. Samia tunaye na tunaenda naye.▪️Asema Rais Samia ni mgombea aliyejipambanua kwa uhodari na uimara wake...
Na. Eva Ngowi, WF, KILIMANJAROSerikali imewaasa wananchi kuepuka kukopa fedha kwenye Taasisi ama vikundi vinavyotoa huduma za kifedha bila...
Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Moshi Mwajuma NAsombe akizungumza wakati wa kikao cha mwisho cha Bajeti cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri...
Na Chedaiwe Msuya, WF, SameWananchi wa Kata ya Kihurio, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuhakikisha wanatumia huduma za Taasisi za...