X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 17/Feb 04:57

MKURUGENZI MOSHI ATOKWA MACHOZI, CCM NA CHADEMA WAKIMPA ZAWADI .

Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Moshi Mwajuma NAsombe akizungumza wakati wa kikao cha mwisho cha Bajeti cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri .Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo akizungumza jambo katika kikao hicho ,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe .Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi wakikabidhi keki kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe kama zawadi kutokana na namna alivyosimamia manispaa hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kufanikisha kupaa kwa mapato ya halmashauri.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akipokea zawadi ya seti ya vyombo kwa ajili ya chakula kutoka kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi kutokana na namna alivyosimamia manispaa hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kufanikisha kupaa kwa mapato ya halmashauri.Diwani wa kata ya Kiboriloni Frank Kagoma (Chadema) akiwaamebeba zawadi ya jagi la kuchemshia chai ikiwa ni zawadi aliyotoa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kutokana na utendajikazi wake .Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akifurahia zawadi ya JAgi alilopewa na Diwani wa kata ya Kiboriloni Frank Kagoma (Chadema) kama zawadi .Na Dixon Hussein - MoshiKatika hatua isiyo ya kawaida katika siasa za Tanzania, diwani pekee wa upinzani katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Frank Kagoma (Chadema) ameungana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kwa usimamizi thabiti wa mapato na miradi ya maendeleo.Mh Kagoma ambaye ni diwani wa kata ya Kiboriloni na viongozi wa CCM wilaya ya Moshi wametoa pongezi hizo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mjini Moshi, ambapo viongozi wa halmashauri hiyo walitangaza ongezeko kubwa la mapato kutoka bilioni 41.7 hadi bilioni 53.2 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24.Katika kikao hicho,Mh Kagoma amekiri kuwa licha ya tofauti za kisiasa, hawezi kupuuza ukweli kwamba usimamizi mzuri wa halmashauri umeleta matokeo chanya kwa wananchi wa Moshi."Mimi ni mpinzani lakini siwezi kupinga maendeleo yanayoonekana. Tumeona miradi ya halmashauri ikitekelezwa kwa wakati, mapato yakiongezeka,hii ni hatua nzuri kwa wananchi," alisema.Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi wakiongozwa na Mwenyekiti wake Faraji Swai pamoja na Madiwani wa CCM wameonyesha furaha yao kwa ufanisi huo, wakisema kuwa halmashauri inatekeleza kwa vitendo ilani ya chama chao kwa kuhakikisha rasilimali zinatumika ipasavyo kwa maendeleo ya wananchi.Mstahiki meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo alisisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya mshikamano kati ya baraza la madiwani, timu ya wataalamu wa halmashauri, na wananchi."Sisi tumejifunza kuwa maendeleo hayana chama. Mkurugenzi wetu amesimamia vyema ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi, na leo tuna bajeti inayotekelezeka kwa zaidi ya asilimia 60, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika miaka ya nyuma," alisema Mwenyekiti huyo.Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akitokwa na machozi amewashukuru viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi kwa kutambua mchango ambao watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wafanya kwa niaba ya wananchi .Hatua hii ya mshikamano wa kisiasa imeibua mjadala mpana kuhusu umuhimu wa kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, huku wadau wa siasa wakisema kuwa inaweza kuwa mfano kwa halmashauri nyingine nchini.

Articles similaires

WAZAZI SHINYANGA MJINI WAPONGEZA UJENZI WA MADARAJA CHIBE - OLD SHINYANGA, IBINZAMATA MAKABURINI

msumbanews.co.tz - 22/Feb 06:19

 Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old ShinyangaWajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika...

NAIBU KATIBU MKUU MWAKITINYA "CCM KUSHINDA SIO OMBI"

msumbanews.co.tz - 19:50

NNaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara (UVCCM), Mussa Mwakitinya amesema ushindi kwa Chama cha Mapinduzi sio ombi...

WANANCHI WAASWA KUKOPA KWENYE VIKUNDI VILIVYOSAJILIWA

msumbanews.co.tz - 14/Feb 12:51

 Na. Eva Ngowi, WF, KILIMANJAROSerikali imewaasa wananchi kuepuka kukopa fedha kwenye Taasisi ama vikundi vinavyotoa huduma za kifedha bila...

KWA KIKOSI HIKI,CCM HII UNAISHINDAJE EEH! UNAISHINDAJE

msumbanews.co.tz - 16/Feb 20:00

Na Dk. Reubeni LumbagalaChama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kikongwe nchini, sasa kimetimiza miaka 48 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977. Ukongwe wa...

MBUNGE RORYA,MWENYEKITI CCM WATUHUMIWA KUGAWA HONGO KWA WAJUMBE MAFUNZO KWA WATENDAJI

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:29

 Wadaia kugawa hongo kati ya Sh.5000 na Sh.50,000 ,Mbunge mwenyewe atoa majibuNa Shomari Binda,RoryaWAKATI joto la uchaguzi ndani ya Chama Cha...

MRISHO GAMBO AFICHUA WIZI MWINGINE NDANI YA JIJI LA ARUSHA

msumbanews.co.tz - 24/Feb 09:19

 Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amefichua taarifa za wizi wa fedha kiasi cha sh252milioni  zilizobambikwa kwenye mahitaji ya manunuzi ya eneo...

RAIS MWINYI:UVCCM ENDELEENI KUHAMASISHA VIJANA CCM ISHINDE NA KUSHIKA DOLA

msumbanews.co.tz - 17/Feb 14:46

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi (CCM)...

FARIKI KWA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME AKIJARIBU KUIBA NYAYA ZA TRANSFOMA SHINYANGA

msumbanews.co.tz - 24/Feb 13:00

 Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya ShinyangaNa Kadama Malunde...

KWENYE URAIS TUMESHAMALIZA-MAJALIWA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:26

▪️Asisitiza Rais Dkt. Samia tunaye na tunaenda naye.▪️Asema Rais Samia ni mgombea aliyejipambanua kwa uhodari na uimara wake...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUTEKELEZA MRADI WA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA NA KATEWAKA

msumbanews.co.tz - 18/Feb 07:46

  ...... Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb.) ameliagiza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kukamilisha majadiliano na...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément