X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 13/Feb 18:11

ULEGA ATAKA WATAALAMU WAKUNE VICHWA KUONDOA KERO YA FOLENI MIJINI

 WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka wataalamu wa wizara hiyo kutumia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Singida kubuni njia zitakapunguza foleni mijini na kuongeza mapato ya serikali. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Baraza hilo, Waziri Ulega alisema pamoja na mkutano huo kuwa na ajenda zake za kawaida kisheria, ni muhimu masuala muhimu kama ya foleni ambayo yanagusa wananchi wengi yakajadiliwa kwa kina kwa sababu mkutano huo umesheheni wataalamu wa kutosha. Akizungumza kwa mifano, Ulega alisema binafsi anaona fursa ya kupunguza kero ya foleni na serikali kujiongezea mapato endapo ubunifu utafanywa kwenye maeneo ambako kuna barabara za mwendokasi. "Hivi hakuna namna ambayo kwa kulipia, magari ya kawaida yanaweza kutumia njia ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) endapo njia za kawaida zitakuwa na foleni? Kwa nini barabara moja ikae nusu saa bila gari kupita wakati kwingine hakuendeki kwa sababu ya foleni? "Kwenye daraja la Mwalimu Nyerere tunafanya hivyo tayari kwa PPP na watu wanalipa kuvuka daraja. Nchi nyingine watu wanalipia kutumia baadhi ya barabara kama hawataki foleni. Naamini tunaweza kufanya kitu lakini tunahitaji wataalamu mtushauri," alisema Ulega.Katika hatua nyingine, Ulega amewaagiza watumishi wa Wizara ya Ujenzi kuhakikisha wanazingatia thamani ya fedha wakati wa utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo barabara, madaraja, vivuko, majengo ya Serikali na viwanja vya ndege. “Nawaelekeza  muendelee kuunga mkono dhamira hii njema ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwenye miradi mnayoisimamia”, amesema UlegaAidha, Ulega ameuagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuongeza juhudi za usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya dharura ya miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua El-Nino na Kimbunga Hidaya yenye thamani ya Shilingi takriban bilioni 868.56.Ameelekeza Viongozi wa Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), kuhakikisha kuwa dhana ya uwezeshaji wa Makandarasi wa ndani inatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili kunufaisha na kuwajengea uwezo makandarasi wazalendo.Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kuendelea kuufungua mkoa wa Singida  kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami ambazo zimesaidia kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji  katika mkoa huo.Naye, Mwenyekiti wa Baraza hilo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi, Aisha Amour amesema kuwa Wizara inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikwemo ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, ujenzi wa daraja la Kigongo- Busisi na ujenzi wa daraja la Mwendokasi (BRT) jijini Dar es Salaam.  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi umefanyika mkoani Singida ambapo ajenda kuu katika Mkutano huo ni kupokea, kujadili na kuidhinisha Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwakawa fedha 2025/26 kabla ya Bajeti hiyo kuwasilishwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kushirikisha wajumbe mbalimbali kutoka Wizarani na Taasisi zilizo chini ya Wizara.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi.

Articles similaires

MWANGA NA WAHIMIZWA KUJISAJILI VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO VYA FEDHA.

msumbanews.co.tz - 17/Feb 08:16

 Na Chedaiwe Msuya, WF, MwangaVikundi vya Kijamii na Huduma Ndogo za Fedha katika Kata ya Lembeni Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, vimetakiwa...

MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA IMEKUWA YA NEEMA JIJINI ARUSHA : GAMBO

msumbanews.co.tz - 19/Feb 10:38

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo, Leo Jumatano Februari 19, 2025 wakati akizungumza na na Wazee wa Wilaya ya Arusha amehimiza...

RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA HALMASHAURI HANDENI, ATOA WITO KWA WATUMISHI KUTOJIVUNIA VYEO

msumbanews.co.tz - 11:40

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Februari 25, 2025 , amezindua rasmi Jengo la Halmashauri ya...

TANZANIA YAPONGEZWA KWA UKUAJI MZURI WA UCHUMI NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:23

 Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, DodomaWashirika wa Maendeleo nchini wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa maendeleo mbalimbali hususan...

BUNGE LAPITISHA NYONGEZA YA BAJETI YA SH. BILIONI 945.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025

msumbanews.co.tz - 14/Feb 14:28

Na. Josephine Majura, WF - Dodoma Bunge limepitisha nyongeza ya mapato na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 945.7 kwa ajili ya kuongeza kwenye...

MRISHO GAMBO AFICHUA WIZI MWINGINE NDANI YA JIJI LA ARUSHA

msumbanews.co.tz - 24/Feb 09:19

 Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amefichua taarifa za wizi wa fedha kiasi cha sh252milioni  zilizobambikwa kwenye mahitaji ya manunuzi ya eneo...

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA WITO KWA WANANCHI WA CHIPOGOLO KUSHIRIKI MAENDELEO

msumbanews.co.tz - 04:58

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe. George Simbachawene akizungumza na...

WAZAZI SHINYANGA MJINI WAPONGEZA UJENZI WA MADARAJA CHIBE - OLD SHINYANGA, IBINZAMATA MAKABURINI

msumbanews.co.tz - 22/Feb 06:19

 Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old ShinyangaWajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika...

ELIMU YA FEDHA, MKOMBOZI WA KIUCHUMI KIJIJI CHA KIHURIO SAME

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:06

 Na Chedaiwe Msuya, WF, SameWananchi wa Kata ya Kihurio, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuhakikisha wanatumia huduma za Taasisi za...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément