X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 19/Feb 05:42

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 16,275 MKOANI SIMIYU

 🎈🎈Mitungi 3,255 yaanza kusambazwa wilayani MaswaMkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi, leo tarehe 18 Februari, 2025 amezindua rasmi zoezi la usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo 6 katika mkoa wa Simiyu na kutoa wito kwa Wananchi kuchangamkia fursa ya matumizi ya nishati safi kama njia mbadala ya kupunguza uharibifu wa mazingira, uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya kuni na mkaa.Mhe. Kenani amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kulinda afya za Watanzania pamoja na kutunza mazingira ambapo amewahamasisha Wananchi wa mkoa wa Simiyu kununua mitungi hiyo ya gesi pamoja na vifaa vyake; mitungi inayosambazwa na kampuni ya ORYX Gas.“Utekelezaji wa Mradi huu, unaunga mkono Mpango Mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo, lengo ni kuhakikisha kuwa angalau asilimia 80 ya Watanzania, wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.” Amesema Mhe. Kihongosi.Usambazaji wa mitungi hiyo ya gesi unatekelezwa kwa pamoja kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na kampuni ya Oryx Gas Tanzania Limited, ambapo Wananchi wanapata fursa ya kukunua mitungi hiyo gesi ya kilo 6 kwa shilingi (20,000); bei ya ruzuku na kiasi kilichobaki kitalipwa na Serikali kupitia REA.Naye Mhandisi wa Miradi ya Nishati Safi kutoka REA, Geofrey Gedo amesema Serikali, imedhamiria kuhakikisha Wanachi waliopo katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji wanatumia nishati safi ya kupikia.“Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetenga fedha, takribani shilingi za Kitanzania milioni 325 kwa ajili ya utekelezaji miradi ya kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia (LPG) kwa mkoa wa Simiyu.“Mradi pia, unalenga katika kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kupunguza ukataji miti, ambapo takribani hekta laki 4 (400,000) hukatwa kila mwaka; wakati asilimia 63.5 ya kaya hutumia kuni kama chanzo kikuu cha nishati na asilimia 26.2 hutumia mkaa.Mhandisi, Gedo ameongeza kuwa mitungi 16,275 itauzwa kwa bei ya punguzo ya asilimia 50 ambayo ni shilingi 20,000 katika mkoa wa Simiyu na kila wilaya ipata mitungi 3,255. Wilaya za mkoa Simiyu zitakazonufaika na usambazaji huo ni pamoja na wilaya ya Maswa, Bariadi, Itilima, Meatu na Busega.Mhandisi, Gedo ameongeza kuwa ili Wananchi wa Simiyu wapate mitungi hiyo wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha NIDA pamoja na shilingi (20,000) na watakapofika katika vituo vya kuuzia mitungi hiyo wataulizwa majina yao, jinsia; namba ya nida; mkoa, wilaya, kata, kijiji na kitongoji /mtaa anapoishi.“Natoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi ili wanunue kwa bei ya punguzo na hata baada ya gesi kuisha; waendelee kutumia nishati safi, ikiwemo gesi.

Articles similaires

TANZANIA KUHUDUMIA NCHI 14 NISHATI YA MAFUTA

msumbanews.co.tz - 17/Feb 16:50

Na Denis Chambi , Tanga.SERIKALI imeanza  mchakato wa uboreshaji wa miundombinu ya Bomba la Tazama  linalosafirisha mafuta kutoka Tanzania hadi...

MAKAMU WA RAIS ATOA WITO KWA WAANDAAJI WA VIPINDI VYA ELIMU KWA UMMA KUHAMASISHA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:32

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 PATO LA SERIKALI KWA KIPINDI CHA MIAKA 4

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:44

Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido akitoa taarifa ya utendaji wa Barrick na Twiga kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 SERIKALINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:23

 • Yachangia Zaidi ya Shilingi Trilioni 11 katika Uchumi wa Tanzania• Gawio la Zaidi ya Shilingi Bilioni 412 latolewa kwa SerikaliKampuni ya...

MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA IMEKUWA YA NEEMA JIJINI ARUSHA : GAMBO

msumbanews.co.tz - 19/Feb 10:38

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo, Leo Jumatano Februari 19, 2025 wakati akizungumza na na Wazee wa Wilaya ya Arusha amehimiza...

BARRICK NI KIELELEZO BORA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI NCHINI- DKT. KIRUSWA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:20

 • Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...

WANANCHI WAASWA KUKOPA KWENYE VIKUNDI VILIVYOSAJILIWA

msumbanews.co.tz - 14/Feb 12:51

 Na. Eva Ngowi, WF, KILIMANJAROSerikali imewaasa wananchi kuepuka kukopa fedha kwenye Taasisi ama vikundi vinavyotoa huduma za kifedha bila...

ZAIDI YA ASILIMIA 40 YA WATUMISHI WA UMMA NCHINI HAWAFANYI KAZI

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:12

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi...

KOROGWE WAIPONGEZA SERIKALI UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME

msumbanews.co.tz - 24/Feb 19:05

 📌 Ni katika ziara ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga📌Vijiji vyote 118 vyafikishiwa umemeWananchi wa Wilaya ya Korogwe wameipongeza...

KIHONGOSI : OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

msumbanews.co.tz - 20/Feb 06:19

Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément