🎈🎈Mitungi 3,255 yaanza kusambazwa wilayani MaswaMkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi, leo tarehe 18 Februari, 2025 amezindua rasmi...
Vous n'êtes pas connecté
Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani Simiyu imeonesha mafanikio makubwa baada ya fisi 16 kuvunwa ikiwa ni hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama na utulivu Kwa wananchi vinarejea.Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.Mhe. Kihongosi amesema kufuatia changamoto hiyo, Serikali ilichukua jukumu kubwa la kuhakikisha inalinda wananchi wake ikiwemo kuanzisha oparesheni maalumu inayohusisha Jeshi la Uhifadhi Kwa Taasisi za TAWA, TANAPA na TFS Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi, oparesheni inayotajwa kuanza Januari 25, 2025."Tarehe 20/12/2024 baada ya fisi kuvamia wananchi Serikali ilichukua hatua kubwa ya kushirikisha vyombo vyake (TAWA na Jeshi la Polisi) na kuanza Oparesheni, lakini ilipofika tarehe 25/01/2025 oparesheni ya mkoa mzima ilifanyika Kwa ukubwa kuhakikisha inakabiliana na fisi wote waliokuwa wanasumbua wananchi" amesema Mhe. Kihongosi "Na Kwa taarifa njema ni kwamba tangu kuanza Kwa oparesheni hii vyombo vyetu vimeweza kudhibiti na kuua fisi 16 na ndio maana kwasasa mnaweza kuona hali imetulia" ameongeza Mkuu huyo wa mkoa wa Simiyu.Aidha Mhe. Kihongosi ameendelea kuwatoa hofu wananchi wa mkoa huo akisisitiza kuwa hali ni shwari na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida huku akikemea vikali imani za kishirikina kuhusiana na mnyamapori aina ya fisi kwa baadhi ya wakazi wa Simiyu na kuwataka wote wanaofuga wanyamapori pori hao kuacha mara moja kwani ni kosa kisheria kumiliki nyara za Serikali bila Kibali.Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amewaomba wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima kuacha tabia ya kutembea nyakati za usiku na alfajiri kwani ni nyakati ambazo wanyama fisi huwa katika mawindo yao.Vilevile amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Jeshi la Uhifadhi waliopo uwandani ili kuongeza ufanisi wa zoezi hilo huku akiwahakikishia kuwa Serikali imedhamiria kulinda wananchi wake na kwamba Askari wapo uwandani wanafanya Kazi usiku na mchana kuwahakikishia usalama wao.Kwa upande wao wananchi wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima wameshukuru Kwa juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo, wakisema kuwa hatua hiyo imeweza kuwarejeshea matumaini, utulivu na amani."Kwakweli tulikuwa tunasumbuliwa sana na haya mafisi ambayo yalikuwa yanauma watu, baada ya Serikali kusikia ikaweka ulinzi, kwakweli imetufanyia vizuri sana mpaka leo hatujawasikia tena tangu Askari waanze kuwashambulia hao fisi, mpaka leo hii tuna utulivu sana kwakweli tunashukuru sana" amesema Mozo Mabula mkazi wa Kijiji cha Mwamunhu kilichopo wilaya ya Itilima.
🎈🎈Mitungi 3,255 yaanza kusambazwa wilayani MaswaMkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi, leo tarehe 18 Februari, 2025 amezindua rasmi...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...
📌Aagiza wasimamiwe kwa karibu kumaliza miradi📌Awataka Watendaji TANESCO kuwa na mahusiano mazuri na wananchiNaibu Waziri wa Nishati, Mhe....
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hatua ya Halmashauri ya Tunduma kutoa...
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya ShinyangaNa Kadama Malunde...
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amemuelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Arusha...
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb) amezitaka Taasisi za Umma ambazo bado...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema zaidi ya asilimia 40 ya Watumishi...
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo (Mb), amezindua rasmi Jengo la Hazina Mkoa wa Geita kwa...
Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ili...