• Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...
Vous n'êtes pas connecté
Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za Afya bila kipingamizi chochote.Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, leo Februari 18, 2025, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, katika kikao cha pamoja na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kilichofanyika ofisi za Wizara, jijini Dodoma.Dkt. Magembe amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kutekeleza vipaumbele mbalimbali vya sekta ya afya, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wote wanakuwa na bima ya afya na uhakika wa matibabu."Kuimarisha mifumo ya taarifa ni hatua muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote unafanikiwa. Mifumo thabiti ya taarifa itawezesha ukusanyaji, uchakataji, na usambazaji wa takwimu sahihi za afya, hivyo kusaidia kufanya maamuzi bora, kufuatilia maendeleo, na kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi," amesema Dkt. Magembe.Aidha, Dkt. Magembe ameeleza kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya afya na faida wanazoweza kupata kupitia mfuko huu.Aidha. Dkt Magembe ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha utekelezaji wa mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote. “Kupitia ushirikiano huu, Tanzania itaweza kutoa huduma bora za afya kwa wananchi na kuwa na mfuko wa bima ya afya jumuishi unaowanufaisha wote, bila kujali hali zao za kiuchumi,” amesema Dkt. MagembeKwa upande wake, Mkuu wa Programu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Bw. Kai Straehler-Pohl amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Ujerumani ni kuhakikisha Serikali ya Tanzania inatekeleza mpango huu kwa ufanisi, ili wananchi wote wapate huduma za afya kupitia mfuko wa bima ya afya."Ushirikiano huu utakuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha hatua zilizosalia zinatekelezwa kwa mafanikio, jambo ambalo litaisaidia nchi kufanikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi kwa wananchi wote," amesema Bw. Kai.
• Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb) amezitaka Taasisi za Umma ambazo bado...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Februari 25, 2025 , amezindua rasmi Jengo la Halmashauri ya...
Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, DodomaWashirika wa Maendeleo nchini wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa maendeleo mbalimbali hususan...
🎈🎈Mitungi 3,255 yaanza kusambazwa wilayani MaswaMkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi, leo tarehe 18 Februari, 2025 amezindua rasmi...
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Jumanne Gombati, amezindua rasmi Bodi mpya ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kuitaka...
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesisitiza kuwa ufungaji wa mgodi wa Buzwagi hautaathiri shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Kahama,...
...... Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb.) ameliagiza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kukamilisha majadiliano na...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefanya mafunzo kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za...