Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...
Vous n'êtes pas connecté
📌Aagiza wasimamiwe kwa karibu kumaliza miradi📌Awataka Watendaji TANESCO kuwa na mahusiano mazuri na wananchiNaibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewataka watendaji wa Sekta ya Nishati kuwajengea uwezo watoa huduma wanaotekeleza miradi mbalimbali ya sekta ya nishati nchini.Hayo ameyasema leo Februari 23, 2025 na Kapinga wakati akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO, na wakuu wa taasisi za wizara kabla ya kushiriki ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kuanza leo mkoani Tanga."Tunataka hii miradi ikamilike kwa wakati na kwa ubora mkubwa, wakandarasi wajengewe uwezo wa utendaji kazi ili kazi ionekane inafanyika, " Ameongeza Mhe. Kapinga. Aidha, ameipongeza REA kwa kumaliza kufikisha umeme kwenye vijiji vyote nchini na kusisitiza miradi inayoendelea na ile inatakayoanza mwaka huu wa fedha itekelezwe kwa wakati. "Ni muhimu sana kuwasimamia wakandarasi kwa nguvu kuanzia mwanzo tuwe nao makini ili miradi hii ya kupeleka umeme kwenye vitongoji ikamilike kwa wakati, " Amesema Mhe. KapingaKatika hatua nyingine, Mhe. Kapinga amewataka watendaji wa taasisi za nishati kuwa na mahusiano mazuri na wananchi hususan wakati wa kupitisha miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao."Imarisheni mahusiano na wananchi mnapopitisha miradi yetu na kuwaeleza kuwa Serikali italipa fidia kwa wote miradi hiyo ilipopita," Amesema Mhe. Kapinga
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)...
Na Josephine Maxime- Dar es Salaam Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko ameagiza Mwanafunzi Mirabelle...
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Kilimo na Maliasili imeipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ubunifu wake katika kuboresha sekta ya utalii...
📌 Ni katika ziara ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga📌Vijiji vyote 118 vyafikishiwa umemeWananchi wa Wilaya ya Korogwe wameipongeza...
🎈🎈Ataka Duru ya Tano ya kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kuwa na matokeo chanya🎈🎈Aipongeza PURA kuwashirikisha...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa...
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka wataalamu wa wizara hiyo kutumia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Singida kubuni njia...
• Tanzania, Rwanda na Uganda zakubaliana kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Kufua Umeme Nsongezi wa 39MWMkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri...
📌 Asema mradi umefikia asilimia 99.8📌 Awaasa watanzania kujivunia mradi wa Julius NyerereKatibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bitekoakizungumza na Watanzania waishio India pamoja na watumishi wa Ubaloziwa Tanzania...