X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 31/Aug 07:39

MIRADI YA NISHATI KUNUFAISHA WANANCHI WANAOIZUNGUKA - KAPINGA

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo yana miradi mikubwa ya nishati watanufaika na miradi hiyo kupitia upatikanaji wa huduma mbalimbali.Mhe. Kapinga amesema hayo  Agosti 30, 2024 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Ally Kasinge Mbunge wa Kilwa Kusini ambaye alitaka kufahamu mkakati wa Serikali katika kuhakikisha Kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi ambako kuna visima vya Gesi Asilia na mitambo ya kuchakata gesi  kinapata umeme wa uhakika."Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa  Nishati, Dkt. Doto Biteko alishatoa maelekezo kuhakikisha wananchi hawa sio tu wanapata umeme wa uhakika bali na huduma nyingine za kijamii ziweze kuimarishwa."Amesema Mhe. Kapinga Amelihakikishia Bunge kuwa, tayari Serikali imeanza kulifanyia kazi  agizo hilo  kwa kuhakikisha wananchi wa Songosongo wanapata umeme wa uhakika na huduma nyingine za kijamii ambazo zinaendana na miradi iliyopo katika maeneo yao.Akizungumzia upelekaji umeme wa gridi kwenye maeneo ya Visiwa, Mhe. Kapinga amesema Tanzania ina visiwa takriban 120 na Serikali imeanza kufanya tathmini ya kufikisha umeme wa gridi katika maeneo hayo.Ameongeza kuwa, kwa sasa visiwa hivyo vinatumia umeme wa jua ambapo Serika imeweka ruzuku ya asilimia 50 hadi 55 ili wananchi wapate umeme wa uhakika kwa muda wote.

Articles similaires

REA KUPELEKA UMEME VISIWA VYOTE TANZANIA BARA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:27

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...

SERIKALI INAENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA KUPELEKA UMEME WA GRIDI MTWARA NA LINDI- MHE.KAPINGA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 10:54

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi wa kuiunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na  umeme wa gridi kutokea...

WAZIRI WA NISHATI ZANZIBAR AIPA KONGOLE REA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:39

 -AISISITIZA KUENDELEA NA UHAMASISHAJI-REA YAELEZEA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINIWaziri wa Maji,...

SERIKALI KUJA NA MRADI WA KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME VITONGOJINI- MHE. KAPINGA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 13:13

Kuhusisha transfoma za kVA50, 100 na 200Vitongoji ambavyo havijapata umeme kufikiwaNaibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali...

REA YAFIKISHA UMEME KWA WANANCHI 2400 NJOMBE

msumbanews.co.tz - 31/Oct 09:15

 Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:22

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...

PUMA ENERGY TANZANIA YATAKIWA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUFANIKISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 16:32

 PUMA Energy Tanzania imetakiwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo mkakati wa...

BASHUNGWA AMPIGIA SIMU KATIBU MKUU AMTAKA KUPIGA KAMBI MAFIA HADI HUDUMA YA USAFIRI WA KIVUKO ITAKAPOREJEA.

msumbanews.co.tz - 28/Oct 07:46

 “Msitoke Mafia mpaka Kivuko kianze kutoa huduma kwa Wananchi”Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amempgia simu na kumuagiza Katibu Mkuu wa...

MIRADI YA TACTIC KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI WA BIASHARA NCHINI- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:02

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...

MTATURU AMPA KONGOLE RAIS SAMIA ASHAURI UWEKEZAJ ZAIDI SEKTA ZA UZALISHAJI

msumbanews.co.tz - 06/Nov 07:02

  MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akichagia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Bajeti ya Serikali...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément