X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 06/Sep 04:47

WAZIRI RIDHIWANI APONGEZA BARAZA LA LESCO KWA UTENDAJI MZURI

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO) kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake.Mhe. Ridhiwani ametoa pongezi hizo leo Septemba 5, 2024 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo wanaomaliza muda wao.“Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa moyo wa dhati kwa kutekeleza vema majukumu yenu kwa ufanisi ili kuhakikisha malengo ya kuanzishwa LESCO yanatimia” amesema.Aidha, amesema katika kipindi cha miaka mitatu, LESCO imefanya kazi nzuri ya kuishauri serikali kuhusu sera zinazohusu masuala ya Ajira na Kazi; upangaji wa kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi; Uridhiaji wa mikataba ya Shirika la Kazi Duniani; na ushirikishwaji wa wadau wa Utatu (Serikali, Waajiri na Wafanyakazi) katika masuala ya kazi, Uchumi na jamii.Ametoa rai kwa wajumbe wa baraza hilo kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuhakikisha sekta ya kazi na ajira inazingatia misingi ya kazi zenye staha kwa maslahi ya wafanyakazi na waajiri.Awali, Mwenyekiti wa LESCO Dkt. Samwel Nyantahe ameishukuru serikali kwa kutoa ushirikiano katikia kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao.Uongozi wa Baraza hilo unamaliza muda wake Septemba 12, 2024 na kwasasa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza mchakato wa kuwapata wajumbe wengine.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhr. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Ushauri wa masuala ya Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO), walipokutana jijini Dodoma leo Septemba 5, 2024.Wajumbe wa Baraza la Ushauri wa masuala ya Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO), wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao cha baraza hilo lililofanyika leo Septemba 5, 2024 jijini Dodoma.Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa masuala ya Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO), Dkt. Samuel Nyantahe akieleza jambo wakati wa kikao cha Baraza hilo lililofanyika leo Septemba 5, 2024 jijini Dodoma.Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mary Maganga akipitia nyaraka wakati wa kikao cha Baraza la Ushauri wa masuala ya Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO), lililofanyika Dodoma, terehe 5 Septemba, 2024.Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Ushauri wa masuala ya Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO), lililofanyika leo Septemba 5, 2024 jijini Dodoma.

Articles similaires

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUZINDUA MFUMO WA MIKOPO WENYE THAMANI YA BILIONI 2.3..

msumbanews.co.tz - 07/Nov 04:30

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua rasmi mfuko wa mikopo wenye kianzio cha shilingi bilioni 2.3...

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

CHANDE AIPONGEZA TIA KWA KUFANIKISHA MBIO ZA MARATHON

msumbanews.co.tz - 26/Oct 17:00

 Na. Scola Malinga, WF, Dar es SalaamNaibu waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa kuandaa...

NAIBU WAZIRI SANGU: e-GA NI TAASISI NYETI KWA USALAMA WA NCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 09:36

  Na. Lusungu Helela Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema  Mamlaka ya Serikali...

MAMENEJA RASILIMALIWATU KATIKA SEKTA YA UMMA AFRIKA WAMUUNGA MKONO RAIS DKT. SAMIA KUTANGAZA SEKTA YA UTALII WA TANZANIA

msumbanews.co.tz - 08/Nov 09:31

Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na...

OUT YATOA MAFUNZO KUIMARISHA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI SERIKALINI

msumbanews.co.tz - 27/Oct 08:36

Mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini yanayoendeshwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa watumishi wa mamlaka za serikali za mitaa pamoja tawala za...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément