Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania TFS imeandaa bonanza la michezo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi mbalimbali kutoka katika kanda zote nane...
Vous n'êtes pas connecté
Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa Mashamba na Wilaya wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutumia Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuboresha utendaji kazi na kuchagiza utawala bora.Ameyasema hayo katika mkutano wa Tatu wa Makamanda wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) uliofanyika leo Novemba 5, 2024 kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha.“Upo ushahidi kabisa kwamba matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA inasaidia kuboresha kazi, utawala bora na kupunguza vitendo vya rushwa ambavyo vingeweza kujitokeza, kuimarisha makusanyo na kudhibiti matumizi ya maduhuli ya serikali” Mhe. Chana amesisitiza.Amewataka Wahifadhi hao kuweka nguvu kwenye kuzuia uhalifu, uharibifu, kutoa elimu, mafunzo na kuweka mabango yanayoonekana katika maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa hasa kwa kutumia mbinu na vifaa vya za kisasa.“Endeleeni kuimarisha ulinzi wa misitu hii kwa kuhakikisha misitu yote inajengwa vituo vya ulinzi hususan sasa na matumizi ya Teknolojia katika ulinzi ambapo changamoto za uhifadhi zinaongezeka, kama kutumia ndege nyuki na satellite” Mhe. Chana amesisitiza.Katika hatua nyingine, Mhe. Chana amewataka wahifadhi hao kufanya kazi kwa uadilifu, weledi wenye mbinu za kijeshi kwa kuzingatia masuala ya haki jinai. Amewataka kutumia fursa za ukuaji wa utalii nchini kuendeleza utalii wa misitu (Forest Based Tourism) na kusisitiza kuwa fursa hiyo ikitumika vizuri itatoa mchango mkubwa katika uhifadhi na kukuza kipato cha jamii na taifa. Awali, Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo amesema lengo la kikao hicho ni kujengeana uwezo wa utendaji kazi, kubadilisha uzoefu, kujadiliana na kushauriana kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za utendaji kazi ili kuimarisha mifumo ya utendaji kazi.Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine kikao hicho kitatoa mada kuhusu Intelijensia ya mawazo, fikra za kimkakati, kujenga uwezo wa kuongoza, usimamizi wa sekta ya misitu , mbinu za uongozi, usimamizi wa sera na sekta ya ufugaji nyuki, changamoto na mwelekeo wake.Kikao hicho kimehudhuriwa na Washiriki takribani 240 ikijumuisha Viongozi wa Kanda zote Saba za TFS pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya TFS, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Deusdedit Bwoyo, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Menejimenti ya TFS, Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa Mashamba na Wilaya wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania TFS imeandaa bonanza la michezo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi mbalimbali kutoka katika kanda zote nane...
Waziri wa Maliasili na Utali,Balozi Dkt Pindi Chana amemwagiza Kamishina wa Wakala wa Huduma na Misitu{TFS},Professa Do Santos Silayo kuhakikisha...
Wakala wa Uhifadhi wa Misitu Nchini (TFS) wameeandaa bonanza la michezo lenye lengo la kujenga mahusiano, ushirikiano na kuhamasisha jamii katika...
Na Denis Chambi, Tanga.MKUU wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani ameuwagiza Wakala wa Maji vijijini 'RUWASA' kuhakikisha wanasimamia...
Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...
Na. Lusungu Helela Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema Mamlaka ya Serikali...
Na : Jusline Marco : ArushaWataalamu wabobezi katika sekta ya Afya wametakiwa wametakiwa kutumia mikakati na mipango waliyoiweka katika kutekeleza...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...
Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Grace Magembe amewaelekeza watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi...