Wakala wa Uhifadhi wa Misitu Nchini (TFS) wameeandaa bonanza la michezo lenye lengo la kujenga mahusiano, ushirikiano na kuhamasisha jamii katika...
Vous n'êtes pas connecté
Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania TFS imeandaa bonanza la michezo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi mbalimbali kutoka katika kanda zote nane nchini kwa lengo la kutoa fursa kwa maafisa uhifadhi kukutana na kubadilishana mawazoKamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Prof. Dos Santos Silayo akizungumza jijini Arusha na waandishi wa habari katika nusu fainali ya bonanza hilo amesema michezo hiyo ni sehemu ya kujenga afya ya akili na mwili Pamoja na kuondoa msongo wa mawazo.Amesema hatua hiyo imetokana na uongozi wa taasisi hiyo kufanya kazi katika mazingira magumu kutokana na majukumu yao ya kazi hivyo kupitia michezo kutawajengea uwezo wa kujiamini na uzalendo sambamba na kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kuweka ari katika kazi ili kuweza kuwafanya wawe na nidhamu katika kazi."Katika kufanya hivi tunalenga kuwakutanisha watumishi wetu kutoka ngazi za chini kabisa na kuweza kufikia kwenye ngazi ya makundi ambapo malengo ni kuongeza idadi ya michezo kwa siku zijazo na idadi ya washiriki kwa kutumia uzoezi ambao tumeupata hapa."Alisema Prof. SilayoAmeongeza kuwa wamekutana kwaajili ya michezo mikuu mitatu ambayo ni Soka,mpira wa Pete pamoja mchezo wa riadha ambapo matarajio yao ni kuongeza michezo mingine zaidi kusudi timu ziweze kuwa nyingi zaidi na kukaa kambia kwa muda mrefu na kupata timu iliyo bora zaidi.Ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo wanategemea TFS itakuwa kinara wa kuonyesha njia katika taasisi za uhifadhi ambazo zinaweza kuletwa pamoja kujenga umoja katika utendaji kazi na kuibua vipaji mbalimbali ikiwemo vya uongozi, kimichezo na kinidhamu katika utendaji wao ambao utawasaidia kuwakuza na kuwalea katika taasisi ili kuweza kulinda rasilimali nyuki,misitu na kuwa wazalendo wa taifa lao wenyewe.Naye Mjumbe wa Bodi TFS Bi. Fiencia Mustapha Kiure amesema uwepo wa wafanyakazi wa TFS fmni faraja kwao na wamefurahishwa na michezo wanayoifanya kwani inawapa faida kubwa ambapo wanayofamefurahishwa kuona jambo hilo linafanyika kwa kukutanisha wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali za nchi kwaajili ya kucheza na kufurahi kwa pamoja.Amesema kuwa mbali na utunzaji wa misitu wanazingatia masuala ya afya kutokana na michezo kuwa sehemu ya afya ya mwili ambapo kupitia michezo hiyo imeweza kuwaleta pamoja wahifadhi kutoka nyanda mbalimbali ili kuweza kujifunza zaidi masuala ya misitu na namna ambavyo wengine wamefanikiwa katika uboreshaji wa misitu na kwenda kutekeleza kwa nafasi zao."Sisi tumejumuika ili tuweze kuona timu mbalimbali na hapa nusu fainali kati ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa zinaendelea kucheza na tunategemea kupata mshindi hapo kesho kwenye fainali kwa upande wa mpira wa miguu na kwa upande wa mpira wa pete vivyo hivyo."alisisitiza Bi.Fiencia Mjumbe wa Bodi TFSSambamba na hayo Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya TFS nchini Enock Emmanuel Nyanda akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kuimarisha ushirikiano, urafiki pamoja na afya ambapo amesema upo umuhimu kwa wafanyakazi kukaa pamoja, kushirikiana na kufanya kazi kwa urafiki.
Wakala wa Uhifadhi wa Misitu Nchini (TFS) wameeandaa bonanza la michezo lenye lengo la kujenga mahusiano, ushirikiano na kuhamasisha jamii katika...
Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...
Waziri wa Maliasili na Utali,Balozi Dkt Pindi Chana amemwagiza Kamishina wa Wakala wa Huduma na Misitu{TFS},Professa Do Santos Silayo kuhakikisha...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza rasmi safari ya kupeleka umeme katika visiwa vyote...
NA ANDREW CHALE.MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na...
Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...
Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...
Na,Jusline Marco : Tanga.Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA kupitia timu zilizopo katika mamlaka hiyo imewasili mkoani Tanga kushiriki katika...
Na,Jusline Marco : Tanga.Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA kupitia timu zilizopo katika mamlaka hiyo imewasili mkoani Tanga kushiriki katika...
Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...