X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 10/Sep 16:13

SERIKALI KUVUTIA WAWEKEZAJI UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI- DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuvutia wawekezaji katika tafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini ili watanzania wanufaike na rasilimali zilizopo.Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 10, 2024 wakati wa Hafla ya makabidhiano ya leseni ya uendelezaji eneo la uzinduzi wa Gesi kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na ARA Petroleum katika kisima cha Ruvuma Ntorya mkoani Mtwara. "Yote haya mnayoyaona ni matunda ya kazi nzuri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan." Amesema Dkt.BitekoAmeongeza kuwa, jitihada za Serikali zinaenda sambamba na kuliwezesha Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ili liweze kushiriki kikamilifu kwenye mnyororo mzima wa thamani wa Mafuta na Gesi.Aidha, ametoa wito kwa TPDC na kampuni ya ARA Petroleum kutoa kipaumbele kwa wazawa  katika utoaji wa ajira ili kuwe na muunganiko kati ya wananchi na ukuaji wa uchumi katika  maeneo hayo.Kuhusu maeneo yenye miradi ya Gesi kama Madimba, Msimbati na Songosongo  amewataka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukamilisha upelekaji wa umeme kwenye maeneo hayo kufikia mwezi Desemba mwaka huu.Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,  Mhe. Kirumbe Ng'enda amesema utoaji wa leseni ya uendelezaji kitalu cha gesi cha Ruvuma ni hatua kubwa  maendeleo nchini. "Kitalu hiki kitazalisha futi za ujazo trilioni 1.6, hili ni jambo kubwa sana na la kuipongeza Serikali, tunampongeza Rais Samia ambaye yeye ndie jemedari wa mapambano ya kuleta maendeleo nchini.' Amesema  Mhe Ng'endaAidha kutokana na uwepo wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere ambao hivi sasa unachangia takribani megawati  705 kwenye gridi ya Taifa, Ng'enda ameiasa Serikali kuwa  gesi hiyo  sasa itoe mchango mkubwa katika nishati safi ya kupikia na katika uendeshaji wa mitambo na kwenye magari.Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,  Mha. Felchesmi Mramba alisema kuwa Tanzania ina historia ndefu katika matumizi ya Gesi Asilia kuanzia miaka ya sabini baada ya ugunduzi katika visiwa vya Songosongo. Ameongeza kuwa,  ugunduzi wa Gesi Asilia umefungua mlango endelevu wa uhifadhi wa mazingira na kuimarika kwa usalama wa nishati.

Articles similaires

DHAMIRA YA RAIS SAMIA NI KUONA WANANCHI WANANUFAIKA NA MIRADI KATIKA MAENEO YAO- KAPINGA

msumbanews.co.tz - 10/Sep 04:08

 Naibu Waziri Nishati, Mhe.  Judith Kapinga amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni...

DKT. BITEKO AHIMIZA WANAWAKE KUTUMIA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

msumbanews.co.tz - 14/Sep 13:14

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanawake nchini kutumia fursa ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi...

WAZIRI MAVUNDE AYATAKA MAKAMPUNI YA MAKAA YA MAWE KUWEKEZA KATIKA UZALISHAJI WA UMEME

msumbanews.co.tz - 05:17

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni za uzalishaji wa makaa ya mawe kwa kuongeza uzalishaji na kuzitaka kuelekeza zaidi...

DKT. BITEKO ASISITIZA MAADILI, WELEDI NA UWAJIBIKAJI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 13:54

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...

RAIS SAMIA ANAAMINI KATIKA USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI -DKT. BITEKO

msumbanews.co.tz - 14:00

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na viongozi wa dini ili kuwawezesha kutimiza...

REA YAENDELEA KUTEKELEZA DHAMIRA YA RAIS SAMIA KWA VITENDO

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:03

Na Mohamed SaifWakala wa Nishati Vijijini (REA) umeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUHUSU SUALA LA UHABA WA FEDHA ZA KIGENI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:35

 Na. Joseph Mahumi na Peter Haule, WF, DodomaSerikali imesema inaendelea kuweka mikakati na mbinu mbalimbali za muda mfupi, wa kati na mrefu katika...

NCHI ZINAZOENDELEA ZINAHITAJI ZAIDI UFADHILI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

msumbanews.co.tz - 03/Sep 05:43

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema unahitajika ufadhili unaotabirika, unaoweza kufikiwa, endelevu na...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément