X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Sep 08:08

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba 11, 2024 jijini Dar es Salaam.Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akitoa elimu ya vipimo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2024.Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akiwaonesha Wahariri na Waandishi wa Habari Tuzo ambayo Wakala hiyo ilitunukiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kuwa miongoni mwa Taasisi zilizofanya vizuri katika utoaji gawio kwa Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024. Taswira hii ilichukuliwa wakati wa kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2024.Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akifafanua kwa Wahariri na Waandishi wa Habari mojawapo ya majukumu ya Wakala hiyo ambayo ni kuhakiki Dira za Maji, wakati wa kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2024.Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile (kulia) na Afisa Habari, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri baada ya kikao baina ya WMA na Wahariri pamoja na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kilichofanyika Septemba 11, 2024 jijini Dar es Salaam.Sehemu ya Wahariri wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2024.Mahamudu Jamal na Pendo Magambo, WMAAfisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla ametoa wito kwa taasisi, asasi na mashirika binafsi kuimarisha ushirikiano na Wakala hiyo katika masuala yanayohusu vipimo kwa nyanja za biashara, afya, usalama na mazingira.Kihulla ametoa wito huo leo Septemba 11, 2024 alipokuwa akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini katika mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, na kufanyika jijini Dar es Salaam.Akitoa taarifa ya utendaji kazi, majukumu pamoja na mafanikio ya WMA, amesema kuwa kuna maeneo zaidi ya 17 ambayo sekta binafsi inaweza kushirikiana na WMA ili kuongeza tija katika sekta ya vipimo nchini.Ametaja baadhi ya maeneo hayo ya kivipimo kuwa ni pamoja na ukaguzi na uhakiki wa mizani, uhakiki wa mitambo ya gesi, dira za maji zilizopo kwenye matumizi, mashine za michezo ya kubahatisha, lifti za majengo na maeneo mengine.Akizungumzia Sheria inayoipa Mamlaka WMA kutekeleza majukumu yake, Mtendaji Mkuu amesema sheria hiyo ambayo msingi wake hasa ni vitabu vitakatifu vya dini Quran na Biblia, ni ya Usimamizi wa Vipimo Sura Namba 245 na 340 ya Mwaka 2002 ambayo inawatambua Maafisa Vipimo kama mainspekta wakati wanapotekeleza majukumu ya ukaguzi na uhakiki wa vipimo.Amebainisha kuwa, jukumu kubwa la WMA ni kuilinda jamii ili kuepukana na madhara yatokanayo na matokeo ya upimaji usio sahihi katika biashara ambapo WMA inawajibika kukagua sehemu za biashara kama vile maduka ya kuuzia bidhaa mbalimbali, viwanda, maduka ya vifaa vya ujenzi, vituo vya kujazia mafuta na sehemu nyinginezo.“Tunasisitiza kila mara kwa wananchi kuwa ukihisi kwamba umepimiwa visivyo sahihi katika sehemu uliyoenda kupata huduma, ni jukumu lako kutoa taarifa ili wataalamu wetu wakafanye uchunguzi eneo hilo.”Aidha, ameongeza kuwa WMA inawajibika kuhakiki mzunguko mzima wa mafuta kuanzia yanapoingia nchini kupitia bandari, uhakiki wa matanki na maghala ya kuhifadhia mafuta ambapo Wakala hufanya shughuli hizo kupitia kitengo maalum cha Bandari “Port Unit”.Sanjari na hayo, Kihulla ameweka wazi kuwa WMA ina mpango wa kuingia kwenye maeneo mapya ya uhakiki wa vipimo kama vile uhakiki wa gharama za vifurushi vya muda wa maongezi na mashine za michezo ya kubashiri (gaming).Pia, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau wa vipimo kuhusiana na matakwa ya sheria ya vipimo, kuendelea kuboresha mifumo ya utendaji kazi pamoja na kuwajengea uwezo zaidi wataalamu wake ikiwa ni kuwapa mafunzo zaidi na ununuzi wa vifaa vya kisasa.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameipongeza WMA kutokana na utendaji kazi wake na ameahidi ushirikiano wa vyombo vya habari na Wakala hiyo ili kuhakikisha elimu ya matumizi sahihi ya vipimo inawafikia wananchi kwa ukubwa wake.“WMA mna nafasi ya kuufikia umma wa watanzania kwa kutumia vyombo vya habari kwenye kampeni hizi za kivipimo, elimu inahitajika sana, wananchi wanatakiwa kufahamu kwamba wanapaswa kuwa makini wanapokwenda kupata huduma mbalimbali, hii itachagiza maendeleo katika taifa letu” amesisitiza Balile.WMA imeendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wadau wake mbalimbali ambao ni pamoja na taasisi za umma na binafsi na pia kuwa mstari wa mbele katika kuchangia katika Pato la Taifa kupitia uwasilishaji wa gawio la Serikali kwa Msajili wa Hazina ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, ilitunukiwa Tuzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Articles similaires

WMA YAHIMIZA USHIRIKIANO KUTOKA SEKTA BINAFSI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 08:08

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...

WMA kutoa gawio la sh. Bilioni 7.7 mwaka wa Fedha 2025/2026

msumbanews.co.tz - 12/Sep 05:50

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari katikq Mkutano mwendelezo ya Mikutano...

WAZIRI JAFO: WIZI WA KUCHEZEA VIPIMO NI KOSA KISHERIA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:50

 WAZIRI  wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amehimiza wananchi jijini Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kila mara wanapofanya...

WMA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA KWA JESHI LA POLISI ILALA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 10:54

  Na Mahamudu Jamal, WMAWakala wa Vipimo (WMA) imekabidhi msaada wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Jeshi la Polisi Mkoa...

WMA YAHIMIZA MATUMIZI YA MIZANI ILIYOHAKIKIWA KWA WAFANYABIASHARA WA GESI

msumbanews.co.tz - 04/Sep 13:38

  Na Pendo Magambo – WMA, Dar es SalaamWakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imewataka wafanyabiashara wa gesi kutumia mizani iliyohakikiwa na WMA ili...

WMA YAHIMIZA MATUMIZI YA MIZANI ILIYOHAKIKIWA KWA WAFANYABIASHARA WA GESI

msumbanews.co.tz - 04/Sep 13:38

  Na Pendo Magambo – WMA, Dar es SalaamWakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imewataka wafanyabiashara wa gesi kutumia mizani iliyohakikiwa na WMA ili...

WMA, TAKUKURU WATEKELEZA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:07

 Na Veronica Simba, WMA DodomaWakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma imetoa elimu ya vipimo kwa Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa...

WAZIRI MAHUNDI AITAKA UCSAF KUTANGAZA SHUGHULI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:11

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano...

WIKI YA AZAKI KUHAMASISHA JAMII KUSHIRIKI DIRA 2050, UCHAGUZI

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:02

 Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society FCS- Justice Rutenge, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini...

AFISA MTENDAJI MKUU DSE AJITAMBULISHA KWA WAZIRI WA FEDHA

msumbanews.co.tz - 04/Sep 14:12

 Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salam (DSE)...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément