X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 09/Sep 07:07

WMA, TAKUKURU WATEKELEZA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA

 Na Veronica Simba, WMA DodomaWakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma imetoa elimu ya vipimo kwa Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), hivyo kutimiza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yanayozitaka Mamlaka na Taasisi za Umma kupanga na kutekeleza kwa pamoja majukumu mbalimbali ya Serikali.Akifungua Semina hiyo ya siku moja iliyofanyika jijini Dodoma, Septemba 6, 2024, Katibu Tawala wa Mkoa, Kaspar Mmuya amepongeza ushirikiano wa Taasisi hizo mbili unaolenga kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais na kuwahudumia wananchi ipasavyo.“Nimefurahishwa na ushirikiano wa Taasisi hizi mbili wenye lengo la kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu dhana ya kufikiri kwa pamoja na kutenda kwa pamoja kama Serikali.”Aidha, Katibu Tawala Mmuya amewataka washiriki kutumia semina hiyo kupambanua endapo kuna mapungufu yoyote katika Sheria ya Vipimo inayosimamiwa na WMA na kutafuta suluhisho la pamoja ili kuboresha utekelezaji wake.Vilevile, amewataka WMA kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wafanyabiashara na walaji ili pande zote mbili zipate kilicho stahiki. Pia, ameongeza kwamba katika utoaji elimu, wakulima waeleweshwe kuachana na utamaduni wa kutumia madalali bali wauze mazao yao katika maghala.“Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo kwamba mazao yauzwe kwenye maghala na huko kwenye maghala kuwe na mizani ambazo zimekaguliwa na kuhakikiwa na Wakala wa Vipimo ili kumlinda mlaji na mfanyabiashara,” ameeleza Mmuya.Mmuya ametoa wito kwa wafanyabiashara, walaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kuzingatia matumizi ya vipimo sahihi na kuwakumbusha kwamba sheria ya vipimo imewapa WMA mamlaka ya kutoza faini kwa yeyote atakayekiuka mwongozo wa sheria hiyo.Amewataka WMA na TAKUKURU kuwa mfano kwa sheria wanazozisimamia na kuchukuliana hatua baina yao endapo kutabainika ukiukwaji wa sheria.“TAKUKURU, mtumishi yeyote wa WMA akitenda ndivyo sivyo kwa kujihusisha na rushwa basi achukuliwe hatua, vivyo hivyo kwa WMA, mkibaini mtumishi wa TAKUKURU anajihusisha na uvunjifu wa sheria ya vipimo katika shughuli zake kama mtanzania wa kawaida ikiwemo kilimo, biashara na nyinginezo, msisite kumchukulia hatua,” amesisitiza.Kwa upande wake, Meneja wa WMA Mkoa wa Dodoma, Karim Zuberi amesema lengo la kutoa semina hiyo kwa watumishi wa TAKUKURU ambao ni watumiaji wa vipimo, ni kuwapatia uelewa ili wajue haki zao wanaponunua bidhaa au kupata huduma mbalimbali.“Kupitia semina hii watapata uelewa ni kwa namna gani kipimo kinatakiwa kuwa kabla, wakati na baada ya kununua bidhaa au kupata huduma,” amesema Zuberi.Vilevile, amesema malengo mengine ni kutekeleza moja ya majukumu ya WMA ambalo ni utoaji elimu ya vipimo kwa jamii kupitia makundi mbalimbali kama wafanyabiashara, viongozi, wanasiasa, watumishi wa umma na mengineyo ambapo TAKUKURU ni kundi mojawapo.Amesema, lengo jingine ni kupata maoni ya TAKUKURU kuhusu namna bora ya kutekeleza sheria ya vipimo endapo watabaini mapungufu wakati wa uwasilishwaji mada katika semina husika.Naye Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Victor Swela ameishukuru WMA kuona umuhimu wa kuandaa semina hiyo ili kuwajengea uelewa wa masuala ya kivipimo hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kiufanisi katika sekta hiyo.“Tutashirikiana na wenzetu wa WMA kuwaelimisha wananchi na kusimamia kuhakikisha kila upande unazingatia matumizi ya vipimo sahihi kwa manufaa ya pande zote yaani wafanyabiashara na walaji.”Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Kaspar Mmuya, akizungumza wakati akifungua semina kuhusu matumizi ya vipimo sahihi iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Dodoma kwa watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Septemba 06, 2024 jijini Dodoma.Meneja, Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma, Karim Zuberi akizungumza wakati wa semina kuhusu matumizi ya vipimo sahihi iliyoandaliwa WMA, kwa watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Septemba 06, 2024 jijini Dodoma.Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma, Victor Swela akizungumza wakati wa semina kuhusu matumizi ya vipimo sahihi iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Dodoma kwa watumishi wa TAKUKURU, Septemba 06, 2024 jijini Dodoma.Sehemu ya watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina kuhusu matumizi ya vipimo sahihi iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Dodoma kwa watumishi wa TAKUKURU, Septemba 06, 2024 jijini Dodoma.

Articles similaires

RUWASA Tanga yaagizwa kusimamia Wananchi kuanzisha vitalu vya miti.

msumbanews.co.tz - 01/Nov 10:58

Na Denis Chambi, Tanga.MKUU wa mkoa wa Tanga  Balozi Dkt. Batilda Buriani  ameuwagiza Wakala wa Maji vijijini 'RUWASA' kuhakikisha wanasimamia...

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

WATAALAM WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA BIASHARA YA KABONI

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:13

Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mafunzo ya...

NAIBU WAZIRI SANGU: e-GA NI TAASISI NYETI KWA USALAMA WA NCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 09:36

  Na. Lusungu Helela Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema  Mamlaka ya Serikali...

EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUACHA KUPIKA TAKWIMU ZA HUDUMA

msumbanews.co.tz - 30/Oct 14:52

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (aliyesimama) akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na...

KONGAMANO LA BIMA YA AFYA KWA WOTE LATOA MAAZIMIO

msumbanews.co.tz - 02/Nov 18:51

 Na : Jusline Marco : ArushaWataalamu wabobezi katika sekta ya Afya wametakiwa wametakiwa kutumia mikakati na mipango waliyoiweka katika kutekeleza...

BILIONI 15 KUSAMBAZA UMEME KWENYE VITONGOJI 105 VYA MKOA WA SIMIYU

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:36

 Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); tarehe 24 Oktoba 2024 imemtambulisha rasmi mkandarasi; kampuni ya CCC (Beijing) Industrial &...

SERIKALI INAENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA KUPELEKA UMEME WA GRIDI MTWARA NA LINDI- MHE.KAPINGA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 10:54

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi wa kuiunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na  umeme wa gridi kutokea...

TANLAP YAWANOA WAANDISHI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 20:57

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu ,Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuripoti Habari kuhusu uchaguzi huo Kwa kuzingatia...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément