X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 30/Oct 14:52

EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUACHA KUPIKA TAKWIMU ZA HUDUMA

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (aliyesimama) akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimdogo. Kulia ni Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira, Mha. Exaudi Fatael Maro na kulia ni Mha. Jovitus Kichum kutoka Wizara ya Maji. Na.Mwandishi Wetu-DODOMA MAMLAKA za Maji na Usafi wa Mazingira nchini zimeelekezwa kutoa taarifa sahihi kuhusu uendeshaji na utoaji wa huduma kwa kuwa taarifa hizo hutumika katika utekelezaji wa mipango ya Serikali inayolenga kuimarisha sekta ya maji nchini. Maelekezo hayo yametolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile, wakati akifungua kikao kazi cha kuhakiki taarifa kwa watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimidogo, jijini Dodoma. Dkt. Andilile alisema kuwa, EWURA imetathmini taarifa zote zilizowasilishwa na Mamlaka hizo katika mfumo wa MajIs kwa Mwaka 2023/24 na kubaini takwimu zisizo sahihi za kiwango cha maji yanayozalishwa, muda wa upatikanaji wa huduma, usimamizi wa usafi wa mazingira,hali ya upatikanaji na kiwango cha uhitaji wa maji,ubora wa maji pamoja na upotevu wa maji. “Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora ya maji na inayokidhi mahitaji yao ya kila siku, tunapokosa takwimu sahihi, ni ngumu kuwapatia wananchi huduma hiyo, hivyo mnatakiwa mtoe kipaumbele katika kuwasilisha takwimu na ziwe sahihi. Kwa upande wake Mhandisi Jovitus Kichum, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, aliwasisitiza watendaji hao kuhakikisha takwimu zinazowekwa kwenye mfumo wa MajIs zinaakisi uhalisia ili Serikali iweze kutatua changamoto zinazojitokeza kwa lengo la kuimarisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira nchini. Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (aliyesimama) akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimdogo. Kulia ni Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira, Mha. Exaudi Fatael Maro na kulia ni Mha. Jovitus Kichum kutoka Wizara ya Maji. Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimidogo wakiendelea kuhakiki taarifa katika mfumo wa MajIs wakati wa kikao kazi kilochoratibiwa na EWURA, jijini Dodoma. Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andillile (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimidogo wakati wa kikao kazi cha kuhakiki taarifa za utendaji wao jijini Dodoma leo 30 Octoba 2024.Wengine ni Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira EWURA, Mha. Exaudi Fatael Maro ( kulia) na Mhandisi. Jovetus Kichum kutoka Wizara ya Maji.

Articles similaires

EWURA YAHAKIKI TAARIFA ZA MAMLAKA ZA MAJI 82 NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:56

Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, Mha. Poline Msuya, akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini, kwa niaba ya...

REA YATOA KIPAUMBELE UJENZI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:22

 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...

RUWASA Tanga yaagizwa kusimamia Wananchi kuanzisha vitalu vya miti.

msumbanews.co.tz - 01/Nov 10:58

Na Denis Chambi, Tanga.MKUU wa mkoa wa Tanga  Balozi Dkt. Batilda Buriani  ameuwagiza Wakala wa Maji vijijini 'RUWASA' kuhakikisha wanasimamia...

NAIBU WAZIRI SANGU: e-GA NI TAASISI NYETI KWA USALAMA WA NCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 09:36

  Na. Lusungu Helela Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema  Mamlaka ya Serikali...

REA YAFIKISHA UMEME KWA WANANCHI 2400 NJOMBE

msumbanews.co.tz - 31/Oct 09:15

 Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...

RAIS DKT. SAMIA AMWAGA AJIRA KWA WAALIMU 29,879

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:27

 Elimu ndio kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kuzingatia hilo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia walimu wapya 29,879 wa Shule za...

ZAIDI YA WANANCHI 32,000 WA VIJIJI VYA WILAYA ZA MOROGORO NA MVOMERO KUANZA KUPATA MAWASILIANO

msumbanews.co.tz - 04/Nov 18:47

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...

WAZIRI KIJAJI AOMBA WWF ISAIDIE KULINDA MAZINGIRA

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:28

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameliomba Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na...

WAANDISHI ZINGATIENI WELEDI, MAADILI, SHERIA NA MIONGOZO UANDISHI WA HABARI ZA UCHAGUZI

msumbanews.co.tz - 06:13

 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa amewataka Waandishi wa Habari nchini kuendelea kutumia weledi, maadili, sheria na...

WAANDISHI ZINGATIENI WELEDI, MAADILI, SHERIA NA MIONGOZO UANDISHI WA HABARI ZA UCHAGUZI

msumbanews.co.tz - 06:13

 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa amewataka Waandishi wa Habari nchini kuendelea kutumia weledi, maadili, sheria na...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément