Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...
Vous n'êtes pas connecté
Elimu ndio kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kuzingatia hilo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia walimu wapya 29,879 wa Shule za Msingi na Sekondari waajiriwe.Uamuzi huo unatokana na nia ya serikali ya kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu nchini.Ikumbuke kuwa tangu Juni, 2021 na Februari 2024, kumekuwa na malalamiko ya uhaba wa waalimu.Walimu hawa wameelekezwa kwenda kutoa huduma kwenye shule mbalimbali nchini, na ujio wao unatajwa kusaidia kupunguza uhaba wa waalimu nchini. Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na Idara mbalimbali za Serikali Kuu (MDAs), ilitangaza nafasi hizo za ajira kwa walimu kwa mwaka 2024. Aidha nafasi 600 za ajira za walimu zilikuwa ni Daraja la III B kwa mwaka 2024, ambazo zilitangazwa na kuwekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na Idara mbalimbali za Serikali Kuu (MDAs) kote nchini na zilitolewa kama sehemu ya mpango wa serikali wa kuboresha sekta ya elimu kwa kuongeza idadi ya walimu wenye sifa ili kuboresha utoaji wa elimu bora nchini.Mwaka 2020/21 hadi mwaka 2022/23, serikali iliweza kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati 10,853.Ikumbukwe kuwa, kwa kipindi kirefu sasa serikali imekuwa katika mchakato wa kuhakikisha inaongeza idadi ya walimu katika shule za msingi na sekondari na Serikali ya awamu ya Sita imelipa kipaumbele. #KAZIINAONGEA
Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Changa, wakijibu maswali ya kuhesabu na kusoma wakati wa tamsha la KKK, lililofanyika shuleni hapo leo 8 Novemba 2024...
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa...
Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) imewezesha mafunzo Walimu Wakuu 17,793 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu...
Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...
Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma Mjini kimeanza mikutano ya ndani ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa mashina(Mabalozi) kuelekea Uchaguzi wa...
Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege kiwanja cha kisasa cha michezo ya...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miradi ya nishati jadidifu nchini ili kusaidia utunzaji wa mazingira, kuzalisha...