X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 07/Nov 09:37

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAELEKEZWA KUFANYA MSAWAZO WA WALIMU

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa walimu kwa kuzingatia bajeti ndani ya Halmashauri ili kutengeneza uwiano sawa kwa shule zote za mijini na vijijini.Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wanchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la Mhe. Emmanuel Mwakasaka mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini aliyetaka kujua serikal inampango gani wa kuhakikisha walimu wanakaa vijijini badala ya kukimbilia Mjini.Akijibu swazi hilo Mhe. Katimba amesema “serikali inatambua kuna changamoto ya walimu kupenda kukaa mijini na kwaniaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI kuwaagiza wakurugenzi wote waweze kuhakikisha kwa kuzingatia bajeti wanaweza kufanya msawazo wa walimu ili kutengeneza uwiano na kuondoa maeneo ambayo yana walimu wengi zaidi na kupelekea maeneo ambayo niya vijijini ambapo hamna walimu kwahiyo wakurugenzi wafanye kazi hiyo” amesemaAwali akijibu swali la Mhe. Mwakasaka linalohusu upungufu wa walimu katika baadhi ya maeneo nchini amesema amesema tayari serikali imetangaza ajira na mwaka huu baada ya mchakato wa ajira watapangiwa vituo vya kazi.

Articles similaires

SERIKALI INAENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA KUPELEKA UMEME WA GRIDI MTWARA NA LINDI- MHE.KAPINGA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 10:54

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatekeleza mradi wa kuiunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na  umeme wa gridi kutokea...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

msumbanews.co.tz - 04/Nov 11:16

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea...

MIRADI YA TACTIC KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI WA BIASHARA NCHINI- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:02

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...

UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA UTAIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA KIGOMA- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:10

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...

CCM WAHIMIZWA KUHAMASISHA WATANZANIA KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO

msumbanews.co.tz - 11/Nov 06:19

 Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

SERIKALI KUJA NA MRADI WA KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME VITONGOJINI- MHE. KAPINGA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 13:13

Kuhusisha transfoma za kVA50, 100 na 200Vitongoji ambavyo havijapata umeme kufikiwaNaibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali...

WATAALAM WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA BIASHARA YA KABONI

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:13

Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mafunzo ya...

SERIKALI YAFAFANUA MSAMAHA WA KODI KWENYE VYAKULA VYA MIFUGO

msumbanews.co.tz - 05/Nov 17:14

 Na. Asia Singano na Peter Haule, WF, Dodoma.Serikali imesema kuwa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani imetoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la...

AICC NI MUHIMILI WA SEKTA YA UTALII NCHINI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:36

 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...

MTATURU AMPA KONGOLE RAIS SAMIA ASHAURI UWEKEZAJ ZAIDI SEKTA ZA UZALISHAJI

msumbanews.co.tz - 06/Nov 07:02

  MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akichagia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Bajeti ya Serikali...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément