X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 31/Oct 08:13

WATAALAM WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA BIASHARA YA KABONI

Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wataalamu wa uhifadhi wa mazingira kutoka katika baadhi ya mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ambazo zimeanza utekelezaji wa miradi itokanayo na biashara ya kaboni, ili kuziwezesha kukabiliana na changamoto kubwa ya uelewa iliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.Bw. Mtwale amesema hayo leo katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma wakati akifungua mafunzo hayo ya siku mbili kwa maafisa na wataalamu wanaosimamia uhifadhi wa mazingira katika mikoa mitano na halmashauri 19 zinazotekeleza miradi ya biashara ya kaboni nchini.“Ninawakumbusha lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi na biashara ya kaboni, hivyo mada mbalimbali zimeandaliwa kuwawezesha kutambua athari za mabadiliko ya tabianchi na pamoja na kujua njia za kuhimili biashara ya kaboni nchini,” Bw. Mtwale amefafanua.Bw. Mtawale amesema kuwa, anatarajia mafunzo hayo yatatoa mwelekeo sahihi wa namna bora ya kuratibu na kutekeleza shughuli mbalimbali za kukabiliana na kuongeza uhimili wa athari za mabadiliko ya tabia nchi.“Hakikisheni mnakuwa na ushirikiano wa kutosha katika kuandaa mipango na bajeti ikiwa ni pamoja na kuandaa miradi ya biashara ya kaboni ili kuimarisha ustawi wa taifa letu,” Bw. Mtwale amesisitiza.Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo, Afisa Maliasili na Mazingira wa Mkoa wa Manyara Bw. Michael Gwandu amesema kuwa, wamepokea mwongozo na maelekezo mahususi ya namna ya kuzingatia mafunzo ya kukabiliana changamoto ya mabadiliko ya tabianchi pamoja na biashara ya kaboni kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya taifa.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa OR-TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta amesema mafunzo hayo yamehudhuriwa na wawakilishi wa mikoa ya Dodoma, Kagera, Manyara, Arusha, Katavi na Ruvuma pamoja na wa halmashauri 19 ambao katika maeneo yao wameanza utekelezaji wa biashara ya kaboni; Mafunzo yatawajengea uwezo na kuwapa fursa ya kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa miradi ya biashara ya kaboni pamoja na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mafunzo hayo ya siku mbili kwa wataalamu wa uhifadhi wa mazingira, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa  jukumu la kusimamia shughuli zote za uhifadhi, utunzaji na usimamizi wa mazingira katika ngazi za mikoa na halmashauri.

Articles similaires

PPPC YAENDESHA MAFUNZO KWA KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI

msumbanews.co.tz - 10:00

 NA EMMANUEL MBATILOKITUO cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha Mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa...

PPPC YAENDESHA MAFUNZO KWA KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI

msumbanews.co.tz - 10:00

 NA EMMANUEL MBATILOKITUO cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha Mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa...

MIRADI YA TACTIC KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI WA BIASHARA NCHINI- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:02

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...

WALIMU WAKUU 17,793 WANOLEWA KUSIMAMIA SHULE KWA UFANISI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 05:54

Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) imewezesha mafunzo Walimu Wakuu 17,793 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu...

UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA UTAIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA KIGOMA- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:10

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

RUWASA Tanga yaagizwa kusimamia Wananchi kuanzisha vitalu vya miti.

msumbanews.co.tz - 01/Nov 10:58

Na Denis Chambi, Tanga.MKUU wa mkoa wa Tanga  Balozi Dkt. Batilda Buriani  ameuwagiza Wakala wa Maji vijijini 'RUWASA' kuhakikisha wanasimamia...

DC MPOGOLO AWATAKA WABUNIFU NA WAKADIRIAJI MAJENZI KUWA WAZALENDO

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:38

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ametoa wito kwa Wabunifu na Wakadiriaji majenzi nchini kuwa Wazalendo, Waadilifu na Wabunifu kwa Taifa katika...

WAZIRI JAFO AWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA KUJA KUJENGA VIWANDA TANZANIA

msumbanews.co.tz - 13:36

  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément