X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 07/Nov 05:54

WALIMU WAKUU 17,793 WANOLEWA KUSIMAMIA SHULE KWA UFANISI

Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) imewezesha mafunzo Walimu Wakuu 17,793 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu uongozi na usimamizi wa Shule.Hayo yamesemwa Novemba 06, 2024 mkoani Katavi na Mkurugenzi wa Elimu ya Awali na Msingi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Abdul Maulid akizungumza katika halfa ya kuhitisha mafunzo hayo kitaifa ambapo amewataka walimu kusimamia ustawi na usalama wa wanafunzi shuleni.‘’Walimu Wakuu ni nguzo muhimu katika sekta ya elimu, naamini mafunzo haya yatawasaidia kujenga mazingira bora ya kufundishia na kujifunza na kukuza vipaji vya wanafunzi’’ alisema Maulid.Aidha ameongeza kuwa, kupitia BOOST Serikali imetumia zaidi ya Sh. Bilioni 230 kuwezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 7,230, matundu ya vyoo 11,297, majengo ya utawala 302 na nyumba za walimu 41’’ alibainisha Maulid. Nae Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya awali na Msingi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mwl. Suzan Nussu amesema inatarajia kuona shule zinaimarika kiutendaji hasa katika eneo la usimamizi na utoaji wa taaluma kwa ujumla, usimamizi na utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Maulid J. Maulid, amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo Walimu Wakuu katika Uongozi na Usimamizi wa Shule pamoja na Utawala Bora kuhakikisha shughuli za ufundishaji na ujifunzaji shuleni zinafanyika kwa ubora na ufanisi unaotakiwa. Wakizungumza kuhusu mafunzo hayo Mkuu wa shule ya msingi Kasekese Mwl. Renatus Benson na  Mwl. Shani Juma Mkuu shule ya msingi Itunya wameishukuru Serikali kuwapatia mafunzo walimu katika wilaya ya Tanganyika, ambapo wameahidi kuyatekeleza kikamilifu.

Articles similaires

TAMASHA LA KKK LAIPAMBA SHULE YA CHANGA TANGA

msumbanews.co.tz - 09/Nov 09:20

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Changa, wakijibu maswali ya kuhesabu na kusoma wakati wa tamsha la KKK, lililofanyika shuleni hapo leo 8 Novemba 2024...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

DC MPOGOLO ATOA MAELEKEZO SIKU YA LISHE

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:31

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameongoza maadhimisho ya Siku ya Lishe Duniani, ambayo kiwilaya yamefantika  katika viwanja vya Shule ya...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA SHULE YA SEKONDARI K/NDEGE DODOMA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 08:44

 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege kiwanja cha kisasa cha michezo ya...

CCM WAHIMIZWA KUHAMASISHA WATANZANIA KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO

msumbanews.co.tz - 06:19

 Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

INEC yawanoa Ma-OCD nchini kuhusu sheria za uchaguzi

msumbanews.co.tz - 08/Nov 06:49

Na Mwandishi wetu, KilimanjaroTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kuhakikisha inatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii,...

RAIS DKT. SAMIA AMWAGA AJIRA KWA WAALIMU 29,879

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:27

 Elimu ndio kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kuzingatia hilo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia walimu wapya 29,879 wa Shule za...

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII

msumbanews.co.tz - 05/Nov 09:20

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...

MTATURU AMPA KONGOLE RAIS SAMIA ASHAURI UWEKEZAJ ZAIDI SEKTA ZA UZALISHAJI

msumbanews.co.tz - 06/Nov 07:02

  MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akichagia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Bajeti ya Serikali...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément