X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 08/Nov 06:49

INEC yawanoa Ma-OCD nchini kuhusu sheria za uchaguzi

Na Mwandishi wetu, KilimanjaroTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kuhakikisha inatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii, leo Novemba 07, 2024 imetoa elimu hiyo kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) nchini katika mafunzo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo ya siku moja kuhusu Sheria mbalimbali na Kanuni zinazoiongoza Tume, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani amesema kwa kuwapa elimu hiyo maafisa hao wa Polisi ngazi ya Wilaya kutasaidia kuondoa migongano baina yao na Vyama vya siasa. “Kimsingi hawa ndio wasimamizi wa sheria ngazi ya Wilaya kutoka Jeshi la Polisi, hivyo tumewapitisha katika Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Rais, Wabunge na Madiwani ili iwawezeshe kuzitafsiri vyema hizi sheria na zitawawezesha katika usimamizi bora wa majukumu yao bila kuleta mtafaruku kati ya chama cha siasa au na wananchi kiujumla,” alisema Bw. Kailima. Kailima amesema kwa sasa Polisi wanajua Wajibu wao ni nini na chama cha siasa kinatakiwa kufanya nini wakati huu ambapo Tume inaendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini. Aidha, Kailima amesema wakati wa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Tume itakutana tena na Jeshi hilo na kuwapa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi Mkuu ili kuendelea kuwa na uchaguzi mkuu wa amani, huru na haki na kuwezesha baada ya uchaguzi Mkuu hali inaendelea kuwa ya utulivu. Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema lengo la mafunzo hayo ni kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa uchaguzi na kwa kuzingatia kuwa wao ndio wasimamizi wa sheria na walinzi wa raia na mali zao wakati wote. CP Awadhi amesema Tume imewapa elimu juu ya wajibu wa Polisi katika shughuli za uchaguzi, sheria na kanuni mbalimbali wakati huu wa uboreshaji na lengo ni kujipanga na kuhakikisha mazoezi yanayoendelea nchini yanafanyika katika hali ya usalama mkubwa. Mafunzo hayo ya siku nne ya Wakuu wa Polisi Wilaya Nchini yaliyoanza Novemba 4, 2024 yanataraji kufikia tamati Novemba 8 mwaka huu ambapo mada mbalimbali kuhusu uchaguzi na ushiriki wa jeshi la Polisi zimetolewa.

Articles similaires

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

RC BATILDA AIPONGEZA HANDENI DC KWA MAANDALIZI MAZURI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

msumbanews.co.tz - 06/Nov 12:16

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dk Batilda Burian amaeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa maandalizi mazuri ya uchaguzi wa Serikali za...

RC MTAKA : NJOMBE TUPO TAYARI KWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 05:03

Mkoa wa Njombe unajiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Uchaguzi huo ni fursa muhimu kwa...

TANLAP YAWANOA WAANDISHI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 08/Nov 20:57

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu ,Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuripoti Habari kuhusu uchaguzi huo Kwa kuzingatia...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

WALIMU WAKUU 17,793 WANOLEWA KUSIMAMIA SHULE KWA UFANISI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 05:54

Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) imewezesha mafunzo Walimu Wakuu 17,793 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu...

WATAALAM WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA BIASHARA YA KABONI

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:13

Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mafunzo ya...

MABALOZI WA CCM BUKOBA MJINI WATUMA SALAAM KWA RAIS SAMIA

msumbanews.co.tz - 08/Nov 19:56

 Semina ya Sheria za Uchaguzi na Vyama Vya Siasa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Ushiriki wa Wanawake katika Siasa  imefanyika Novemba 7...

BARAZA LA MAWAZIRI SASA KIDIJITALI-MAJALIWA

msumbanews.co.tz - 12:08

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza la Mawaziri utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta...

BARAZA LA MAWAZIRI SASA KIDIJITALI-MAJALIWA

msumbanews.co.tz - 12:08

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza la Mawaziri utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément