X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 01/Nov 09:27

RAIS DKT. SAMIA AMWAGA AJIRA KWA WAALIMU 29,879

 Elimu ndio kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kuzingatia hilo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia walimu wapya 29,879 wa Shule za Msingi na Sekondari waajiriwe.Uamuzi huo unatokana na nia ya serikali ya kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu nchini.Ikumbuke kuwa tangu Juni, 2021 na Februari 2024, kumekuwa na malalamiko ya uhaba wa waalimu.Walimu hawa wameelekezwa kwenda kutoa huduma kwenye  shule  mbalimbali nchini, na ujio wao unatajwa kusaidia kupunguza uhaba wa waalimu nchini. Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na Idara mbalimbali za Serikali Kuu (MDAs), ilitangaza nafasi hizo za ajira kwa walimu kwa mwaka 2024. Aidha nafasi 600 za ajira za walimu zilikuwa ni Daraja la III B kwa mwaka 2024, ambazo  zilitangazwa na kuwekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na Idara mbalimbali za Serikali Kuu (MDAs) kote nchini na zilitolewa kama sehemu ya mpango wa serikali wa kuboresha sekta ya elimu kwa kuongeza idadi ya walimu wenye sifa ili kuboresha utoaji wa elimu bora nchini.Mwaka 2020/21 hadi mwaka 2022/23, serikali iliweza kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati 10,853.Ikumbukwe kuwa, kwa kipindi kirefu sasa serikali imekuwa katika mchakato wa kuhakikisha inaongeza idadi ya walimu katika shule za msingi na sekondari na  Serikali ya awamu ya Sita imelipa kipaumbele. #KAZIINAONGEA

Articles similaires

CCM WAHIMIZWA KUHAMASISHA WATANZANIA KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO

msumbanews.co.tz - 11/Nov 06:19

 Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

TAMASHA LA KKK LAIPAMBA SHULE YA CHANGA TANGA

msumbanews.co.tz - 09/Nov 09:20

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Changa, wakijibu maswali ya kuhesabu na kusoma wakati wa tamsha la KKK, lililofanyika shuleni hapo leo 8 Novemba 2024...

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAELEKEZWA KUFANYA MSAWAZO WA WALIMU

msumbanews.co.tz - 07/Nov 09:37

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa...

WALIMU WAKUU 17,793 WANOLEWA KUSIMAMIA SHULE KWA UFANISI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 05:54

Serikali kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) imewezesha mafunzo Walimu Wakuu 17,793 katika Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuhusu...

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA WADAU KUJIKITA VIJIJINI, ELIMU YA KUPINGA UKATILI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:24

  Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...

CCM DODOMA MJINI YAANZA KUWANOA MABALOZI KUJIANDAA NA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

msumbanews.co.tz - 06/Nov 16:57

Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma Mjini kimeanza mikutano ya ndani ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa mashina(Mabalozi) kuelekea Uchaguzi wa...

SERIKALI ITAENDELEA KUWATUMIA WATAFITI NCHINI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 16:47

 Na : Jusline Marco : ArushaWaziri wa nchi,ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawane amesema serikali ya...

MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA SHULE YA SEKONDARI K/NDEGE DODOMA

msumbanews.co.tz - 04/Nov 08:44

 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege kiwanja cha kisasa cha michezo ya...

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

UINGEREZA KUSAIDIA TANZANIA SEKTA YA AFYA

msumbanews.co.tz - 12/Nov 15:13

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam.Tanzania na Uingereza zimesaini hati za Makubaliano ya nyongeza ya kuchangia Mfuko wa Kusaidia Sekta ya Afya...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément