X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Sep 07:50

WAZIRI JAFO: WIZI WA KUCHEZEA VIPIMO NI KOSA KISHERIA

 WAZIRI  wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amehimiza wananchi jijini Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kila mara wanapofanya manunuzi na kuuza bidhaa mbalimbali.Aliyasema hayo Septemba 11, 2024 wakati akifungua rasmi Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza."Wizi wa kuchezea vipimo ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na. 340 na hata vitabu vya dini vinakataza wizi wa vipimo," alisisitiza.Katika hatua nyingine, akizungumzia ushiriki wa Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho hayo, Afisa Vipimo Mwandamizi Mkoa wa Mwanza, Lazaro Joram alisema ni mwendelezo wa utoaji elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya vipimo kwa wafanyabiashara waliopo ndani ya Mkoa wa Mwanza pamoja na nchi jirani."WMA tunatumia Maonesho haya ili kuwawezesha wadau wetu kutambua majukumu yetu, kueleza umuhimu wa kuhakiki na kutumia vipimo sahihi na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi ya vipimo pamoja na kuendelea kuwaelimisha kuhusu aina za vipimo vinavyopaswa kutumika katika biashara."Joram aliwakaribisha wananchi kutembelea Banda la WMA ili kufahamu aina za mizani wanazoweza kutumia katika sekta za kilimo, uvuvi, biashara na usafirishaji.“Tunazo aina nyingi za mizani lakini siyo kila mzani unaruhusiwa kutumika katika biashara au katika sekta ya kilimo hivyo ukitembelea Banda letu tutakupa elimu ya kutambua mizani sahihi iliyohakikiwa pamoja na kutambua alama zinazowekwa katika vipimo vilivyo hakikiwa,” alisema.Akidadavua kuhusu elimu inayotolewa kwa wananchi wanaotembelea Banda la WMA, Joram alisema eneo mojawapo ni kuhusu namna sahihi ya ufungashaji wa mazao ya shamba ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo mazao yote yanatakiwa kufungashwa kwa uzito usiozidi kilogramu mia moja (100 kg) na endapo mkulima atafungasha mazao kwa uzito zaidi ya uliotajwa kisheria atakuwa amefungasha Lumbesa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.“Kwa sasa tafsiri ya lumbesa ni uzito unaozidi kilo mia moja (100 kg) tofauti na awali ambapo ilikuwa inatafsiriwa kama kuongeza kifungashio juu ya gunia hivyo tunawahimiza wakulima kutumia mizani ili kujua uzito wa mazao wanayofungasha,” alisisitiza.Akieleza zaidi, alisema kuwa, Kanda ya Ziwa kuna mazao ya kimkakati aina mbili ambayo ni Pamba na Kahawa ambapo jukumu la WMA ni kuhakiki mizani zote zinazotarajiwa kutumika kwenye ununuzi wa mazao hayo kabla ya msimu kuanza na baada ya kufanya uhakiki mizani iliyo sahihi huruhusiwa kutumika katika ununuzi wa mazao hayo.Vilevile, alisema wakati wa ununuzi, WMA hufanya kaguzi za kushtukiza katika Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ili kujiridhisha kama mizani zinatumika kwa usahihi kama zilivyo hakikiwa ili kuwalinda wakulima.Pamoja na majukumu mengine, WMA pia ina jukumu la kusimamia usahihi wa vipimo kwenye sekta ya usafirishaji ambao ni pamoja na usafiri wa anga, barabara na usafiri wa majini kwa kuhakikisha mizani zinazotumika ziko sahihi na zimehakikiwa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kubeba mizigo yenye uzito mkubwa ambayo inaweza kusababisha vyombo hivyo kuanguka na miundombinu kuharibika.Kwa upande wake, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WMA anayeshiriki Maonesho hayo, Paulus Oluochi alitoa wito kwa wananchi kutembelea Banda la WMA ili kujifunza kuhusu matumizi sahihi ya vipimo lakini pia kuwasilisha changamoto mbalimbali kama zipo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.Alisema endapo mwananchi yupo mbali, anaweza kuwasiliana na WMA kupitia nambari isiyo na malipo 0800 110097.Maonesho hayo ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanatarajiwa kufikia tamati Septemba 15, 2024.Afisa Vipimo Mwandamizi Mkoa wa Mwanza, Lazaro Joram (kulia) akitoa elimu ya vipimo kwa wadau waliotembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi Septemba 10, 2024 na yanatarajiwa kuhitimishwa Septemba 15, 2024.

Articles similaires

WAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:01

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2024) amefanya ziara jijini Dodoma ili kukagua utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi...

SERIKALI YAWASIHI WANANCHI KUTUMIA ELIMU YA FEDHA ILI KUKUZA UCHUMI

msumbanews.co.tz - 26/Oct 16:56

 Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Mbeya.Wakazi wa Jiji la Mbeya wametakiwa kutumia elimu waliyoipata katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma...

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

WATAALAM WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA BIASHARA YA KABONI

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:13

Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeandaa mafunzo ya...

KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA KULETA UWEKEZAJI NA UBUNIFU MPYA TANZANIA -MHE. KADUARA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:49

 Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Shaibu Kaduara amesema Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi Afrika...

MAKAMANDA TFS WATAKIWA KUTUMIA TEHAMA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

msumbanews.co.tz - 05/Nov 14:13

 Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...

KONGAMANO LA BIMA YA AFYA KWA WOTE LATOA MAAZIMIO

msumbanews.co.tz - 02/Nov 18:51

 Na : Jusline Marco : ArushaWataalamu wabobezi katika sekta ya Afya wametakiwa wametakiwa kutumia mikakati na mipango waliyoiweka katika kutekeleza...

INEC yawanoa Ma-OCD nchini kuhusu sheria za uchaguzi

msumbanews.co.tz - 06:49

Na Mwandishi wetu, KilimanjaroTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kuhakikisha inatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii,...

EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUACHA KUPIKA TAKWIMU ZA HUDUMA

msumbanews.co.tz - 30/Oct 14:52

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (aliyesimama) akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na...

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUZINDUA MFUMO WA MIKOPO WENYE THAMANI YA BILIONI 2.3..

msumbanews.co.tz - 07/Nov 04:30

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua rasmi mfuko wa mikopo wenye kianzio cha shilingi bilioni 2.3...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément