X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 26/Oct 16:56

SERIKALI YAWASIHI WANANCHI KUTUMIA ELIMU YA FEDHA ILI KUKUZA UCHUMI

 Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Mbeya.Wakazi wa Jiji la Mbeya wametakiwa kutumia elimu waliyoipata katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kitaifa kubadilisha maisha yao hususan katika masuala ya usimamizi wa fedha.Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, wakati akifunga maadhimisho hayo Jijini Mbeya.Dkt. Mwamwaja alisema kwamba elimu waliyoipata inatakiwa iwabadilishe kwa kuacha mambo yote waliyokuwa wakiyafanya awali kwa kufuata utaratibu na maamuzi sahihi wanaposhighulikia masuala yao ya kifedha.“Wataalam wanasema mikopo siyo mibaya, lakini kabla hujakopa lazima uwe na malengo, usikope kwa sababu fedha zipo mahala fulani, ukope ukiwa na mpango. Naamini hii ni sehemu mojawapo ya kubadilika”, alisisitiza Dkt. Mwamwaja.Alisisita wananchi wanapochukua mikopo wahakikishe wanasoma mikataba na kuchukua nakala za mikataba hiyo ili kuepuka madhara mbalimbali yanayotokana na mikop yenye masharti magumu maarufu kama mikopo umiza. Dkt. Mwamwaja pia alitoa rai kwa wananchi hao kutumia huduma rasmi za fedha kwa kuhakikisha kila wanachokifanya katika shughuli zao za masuala ya kifedha ziwe zimerasimishwa.“Kama ni kikoba ni jambo zuri na kinaungwa mkono lakini hicho kikoba kisajiliwe ili kiwe rasmi”, aliongeza Dkt. Mwamwaja.Aliwasihi kutumia elimu waliyoipata kuwaelimisha wengine ambao hawakuweza kufika katika maadhimisho hayo kwa kuwa elimu ya fedha ni endelevu na haitolewi kwenye maadhimisho hayo pekee. Aidha, alisema utoaji wa elimu ya fedha ni endelevu ingawa utoaji wa elimu hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa hutolewa mara moja kwa mwaka. “Maadhimisho haya ambayo tunamaliza leo sio mwisho wa kutoa elimu, bado tutaendelea na kutumia njia mbalimbali katika kutoa elimu ya fedha, tusitoke hapa tukasema baada ya maadhimisho haya fursa hii ya kutoa elimu inafungwa hadi mwakani, Hapana. Utoaji wa elimu ya fedha ni endelevu”, alisema Dkt. Mwamwaja.Alisema Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeteua Waratibu wa Huduma Ndogo za Fedha katika kila mkoa na halmashauri nchini ambao wamekuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi.Maadhimisho hayo ni ya nne kufanyika nchini ambayo ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 na yanalenga kutoa elimu ya fedha kwa umma na kuongezeka kwa mchango wa Sekta ya Fedha kwenye ukuaji wa Uchumi.

Articles similaires

SERIKALI YAFIKIA ASILIMIA 85 KATIKA UPATIKANAJI WA DAWA

msumbanews.co.tz - 31/Oct 08:32

 Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...

TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

msumbanews.co.tz - 13:07

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...

TANZANIA NA EU KUIMARISHA USHIRIKIANO

msumbanews.co.tz - 13:07

 Na. Joseph Mahumi, WF, Dar es SalaamTanzania imeishukuru Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuendelea kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa kimkakati wa...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 07/Nov 15:02

 Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...

KONGAMANO LA BIMA YA AFYA KWA WOTE LATOA MAAZIMIO

msumbanews.co.tz - 02/Nov 18:51

 Na : Jusline Marco : ArushaWataalamu wabobezi katika sekta ya Afya wametakiwa wametakiwa kutumia mikakati na mipango waliyoiweka katika kutekeleza...

TATHIMINI YA USIMAMIZI WA HUDUMA ZA AFYA MSINGI KUFANYIKA KILA BAADA YA WIKI MBILI - Dkt. Magembe

msumbanews.co.tz - 13:31

 Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Grace Magembe amewaelekeza watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi...

TATHIMINI YA USIMAMIZI WA HUDUMA ZA AFYA MSINGI KUFANYIKA KILA BAADA YA WIKI MBILI - Dkt. Magembe

msumbanews.co.tz - 13:31

 Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMINaibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Afya) Dkt. Grace Magembe amewaelekeza watumishi wa Idara ya Afya, Ustawi...

CHANDE ASHAURI MABENKI KUTANUA WIGO WA MASOKO NJE YA NCHI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:25

 Na. Peter Haule na Josephine Majura, WF, Dodoma Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameitaka Akiba Commercial Bank Plc (ACB)...

EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUACHA KUPIKA TAKWIMU ZA HUDUMA

msumbanews.co.tz - 30/Oct 14:52

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (aliyesimama) akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na...

Wagonjwa wa moyo kutoka Malawi kutibiwa JKCI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:38

 Serikali ya Jamhuri ya Malawi imeahidi kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili wagonjwa wa moyo waliopo nchini humo hasa watoto...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément