Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), ametembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote...
Vous n'êtes pas connecté
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutumia vyombo vya habari ili kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Mhandisi Mahundi amesema hayo tarehe 10 Septemba, 2024, wakati wa ziara yake katika ofisi za UCSAF Kanda ya Pwani zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua shughuli mbalimbali pamoja na mradi wa Tanzania ya Kidijitali wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini.“Mahusiano na vyombo vyetu vya habari ni muhimu, Ukifanya kazi ukikaa nayo, hakuna atakayejua umefanya hivyo. Ni muhimu kuvishirikisha katika utekelezaji wa shughuli zenu mbalimbali,” amesisitiza Mhandisi Mahundi.Aidha, Naibu Waziri huyo amehimiza UCSAF kuwashirikisha viongozi mbalimbali, wakiwemo wabunge, wanapotoa huduma za mawasiliano katika maeneo yao.Amesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia katika kupata taarifa sahihi za maendeleo katika maeneo husika.Katika hatua nyingine, Mhandisi Mahundi amesisitiza umuhimu wa kuongeza kasi katika ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, akieleza kuwa kumekuwa na mahitaji makubwa ya mawasiliano katika maeneo mengi.Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema tayari wameshakaa kikao na kampuni za simu na kuweka utaratibu mzuri wa kukamilisha ujenzi wa minara hiyo, pamoja na kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli zinazofanywa na mfuko huo.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), ametembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote...
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea...
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea...
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...
Katika muendelezo wa hamasa ya wananchi wa Ngorongoro kujiandikisha kuhama kwa hiari, leo tarehe 7 Septemba, 2024 jumla ya kaya 58 zenye wananchi 228...
Waziri wa Ujenzi,Innocent Bashungwa amewataka Wahandisi kuwajibika katika majukumu pale wanapopatiwa mradi ili kulinda thamani yao. Akizungumza...
Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi,...