X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 08/Sep 07:50

WANANCHI WENGINE 228 WAHAMA NGORONGORO

Katika muendelezo wa hamasa ya wananchi wa Ngorongoro kujiandikisha kuhama kwa hiari, leo tarehe 7 Septemba, 2024 jumla ya kaya 58 zenye wananchi 228 na mifugo 350 wamehama katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera na maeneo mengine waliyochagua katika wilaya za Monduli, Meatu na Simanjiro.Akitoa taarifa wakati wa kuaga kundi la 19 la awamu ya pili linalohama kutoka hifadhi ya Ngorongoro, Meneja mradi wa kuhamisha wananchi wa Ngorongoro Afisa Uhifadhi Mkuu Flora Assey ameeleza kuwa, kati ya kaya  58 zilizohama leo, kaya 30 zenye watu 151 na mifugo 235 zinahamia Kijiji cha Msomera,  Kaya 28 zenye watu 78 na mifugo 115 zinakwenda maeneo mengine waliyochagua katika wilaya za Monduli Mkoani Arusha,  Meatu mkoani Simiyu na Simanjiro katika mkoa wa Manyara.Amebainisha kuwa tangu zoezi la kuhamisha wananchi kwa hiari lilivyoanza mwezi Juni 2022 hadi kufikia leo Septemba 7, 2024 Jumla ya kaya 1,627 zenye watu 9,778 na mifugo 40,051 zimeshahama ndani ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro.“Tunawapongeza sana kwa maamuzi ya kuhama hifadhini kwa ajili ya kupisha shughuli za uhifadhi, maeneo mnayohamia Serikali imeshawajengea huduma muhimu kama shule, zahanati, maji, majosho, mawasiliano, nishati ya umeme, makazi bora pamoja na mashamba ya kilimo na malisho. Pamoja na zoezi hili la kuhama kuendelea, niwahakikishie wananchi ambao bado hawajaamua kuhama kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma za kijamii na katika utekelezaji wa zoezi hili tutaendelea kuzingatia misingi ya sheria, kanuni, taratibu na haki za binaadamu” aliongeza Hamza.Akizungumza kwa niaba ya wananchi wanaohama kwa hiari, Elizabeth Saiboko kutoka Kijiji cha Nainokanoka amebainisha kuwa ameamua kuhama ndani ya hifadhi ili kuwa huru zaidi na kutafuta kesho iliyobora kwa watoto wake kwa kuwa katika tarafa ya Ngorongoro sheria za uhifadhi zinauiya baadhi ya shughuli za kiuchumi kama kilimo, ujenzi wa nyumba za kudumu, kumiliki vyombo vya moto na uhuru wa kutembea  kwa saa 24 tofauti na maeneo mengine nje ya hifadhi.

Articles similaires

ZOEZI LA KUHAMA KWA HIARI LIPO PALEPALE - WAZIRI CHANA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:54

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amesisitiza kuwa zoezi la kuhama kwa hiari kwa wananchi wa Ngorongoro linaendelea...

ZOEZI LA KUHAMA KWA HIARI LIPO PALEPALE - WAZIRI CHANA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:54

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amesisitiza kuwa zoezi la kuhama kwa hiari kwa wananchi wa Ngorongoro linaendelea...

ASKARI UHIFADHI NGORONGORO WATAKIWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:13

 Askari Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) wametakiwa kujenga mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka Hifadhi ya...

ASKARI UHIFADHI NGORONGORO WATAKIWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WANANCHI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 15:13

 Askari Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) wametakiwa kujenga mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka Hifadhi ya...

TANAPA yaanza na mkakati wa kuboresha barabara zilizopo Hifadhi za Taifa hususani barabara ya Serengeti

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:02

 WADAU wa Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wameiomba Serikali kupatia suluhisho la kudumu la ujenzi wa barabara katika Hifadhi za Taifa...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

WAHIFADHI TFS-SHAMBA LA MITI SAOHILL WAPONGEZWA KWA UTENDAJI KAZI MZURI

msumbanews.co.tz - 10/Sep 14:28

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewapongeza wahifadhi Shamba la Miti la Miti Saohill kwa utekelezaji mzuri wa...

DKT. BITEKO AAGIZA KIGOMA KUINGIZWA KWENYE GRIDI KABLA YA 2025

msumbanews.co.tz - 16:02

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linatekeleza kwa kasi...

DC MPOGOLO ATAKA VIONGOZI KUWA NA MAHUSIANO MEMA

msumbanews.co.tz - 05:50

 Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi wa chama na serikali kuwa na mahusiano mazuri katika kazi zao.Akiongea na viongozi wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément