Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), ametembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote...
Vous n'êtes pas connecté
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutumia vyombo vya habari ili kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.Mhandisi Mahundi amesema hayo tarehe 10 Septemba, 2024, wakati wa ziara yake katika ofisi za UCSAF Kanda ya Pwani zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua shughuli mbalimbali pamoja na mradi wa Tanzania ya Kidijitali wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini.“Mahusiano na vyombo vyetu vya habari ni muhimu, Ukifanya kazi ukikaa nayo, hakuna atakayejua umefanya hivyo. Ni muhimu kuvishirikisha katika utekelezaji wa shughuli zenu mbalimbali,” amesisitiza Mhandisi Mahundi.Aidha, Naibu Waziri huyo amehimiza UCSAF kuwashirikisha viongozi mbalimbali, wakiwemo wabunge, wanapotoa huduma za mawasiliano katika maeneo yao.Amesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia katika kupata taarifa sahihi za maendeleo katika maeneo husika.Katika hatua nyingine, Mhandisi Mahundi amesisitiza umuhimu wa kuongeza kasi katika ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, akieleza kuwa kumekuwa na mahitaji makubwa ya mawasiliano katika maeneo mengi.Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema tayari wameshakaa kikao na kampuni za simu na kuweka utaratibu mzuri wa kukamilisha ujenzi wa minara hiyo, pamoja na kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli zinazofanywa na mfuko huo.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), ametembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote...
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea...
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea...
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa...
Kampuni ya simu za mkononi Airtel kupitia kwa Mkurugenzi wa Biashara Joseph Muhele amesema kuwa mtandao huo mwaka huu 2024 unaendelea kufangua...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...
Mkurugenzi wa Ufundi na Undelezaji kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL,Mhandisi Cecil Francis ameeleza kuwa wamefanikiwa kuunganisha wilaya...
Na Mwandishi Wetu, Moshi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewataka Watanzania kuacha mara moja tabia ya...
Katika muendelezo wa hamasa ya wananchi wa Ngorongoro kujiandikisha kuhama kwa hiari, leo tarehe 7 Septemba, 2024 jumla ya kaya 58 zenye wananchi 228...