X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 19/Sep 18:34

MSIUZE MAENEO YA WAZI - PINDA

  Na Mwandishi Wetu, Moshi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewataka Watanzania kuacha mara moja tabia ya kuuza maeneo ya wazi ili kuhifadhi ardhi kwa matumizi ya dharura na maeneo mbadala yanapohitajika. Mhe. Pinda amesema hayo katika kikao cha wananchi na watumishi wa Ardhi Mkoa wa Kilimanjaro kilichofanyika Septemba 19, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo. Maeneo ya wazi yana faida kubwa kwa kwa jamii ikizingatiwa hutoa huduma za jamii wakati wa dharura inapojitokeza na kutumika kulingana na mahitaji ikiwamo ujenzi wa vituo vya Afya, maeneo ya biashara na ujenzi wa vituo vya kutolea elimu katika shule mbalimbali.   "Maeneo haya ya wazi niwasihi watanzania wenzangu muendelee kutayatumia kwa vibali vya Mkurugenzi, tutafanyia wapi biashara ndogo ndogo? Kwa sababu hata tukiuza hawa watoto wetu na wajukuu watafanyia biashara wapi? Muungane na mimi maeneo ya wazi tusiweke wazo la kuyauza" amesema Mhe. Pinda. Mhe. Pinda amelipongeza Baraza la Madiwani la Halimashauri ya Moshi Mjini kwa msimamo wao imara wa kuzuia uuzaji wa maeneo ya wazi. "Nawashukuru sana Waheshimiwa madiwani mna madiwani wana misimamo thabiti, wamesimama imara baadhi ya maeneo kutoyaruhusu yauzwe, mfano lile eneo la gerage" amesema Naibu Waziri Pinda. Aidha, Mhe. Pinda amewaonya Maafisa Ardhi wasio waaminifu na weledi kwa taaluma zao na kujihusisha na ugawaji kiwanja  kimoja mara mbili na kusisitiza kuwa Wizara itachukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya mtumishi atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma kwa taaluma yake. "Kama litamhusisha Afisa wa kwetu kwenye jambo la kugawa kiwanja kimoja mara mbili, sasa hivi hatunamswalia Mtume tutachukua hatua kali" amesema Naibu Waziri Pinda. Naibu Waziri Mhe. Pinda yuko katika ziara ya kikazi mkoni Kilimanjaro ambapo mbali na mambo mengine atasikiliza na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na kufanya vikao kazi na watumishi wa Ardhi mkoani humo.

Articles similaires

PINDA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI DODOMA

msumbanews.co.tz - 01/Nov 18:00

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemaliza mgogoro wa Ardhi wa Familia ya Bw. Emmanuel Corneli Mbunda na Mzee...

PINDA ASHIRIKI MAZISHI KUMUAGA JAJI KIPENKA

msumbanews.co.tz - 07/Nov 04:34

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Mizengo Pinda ameshiriki mazishi ya kuuanga Mwili wa  marehemu Jaji Kipenka...

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBU YA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

msumbanews.co.tz - 04/Nov 11:16

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombu ya kutolea...

MIRADI YA TACTIC KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI WA BIASHARA NCHINI- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:02

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema kukamilika kwa Miradi ya TACTIC mkoani...

UJENZI WA SOKO LA MWANGA NA KATONGA UTAIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA KIGOMA- MHE. KATIMBA.

msumbanews.co.tz - 02/Nov 16:10

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amesema ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanga na Soko la...

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAELEKEZWA KUFANYA MSAWAZO WA WALIMU

msumbanews.co.tz - 07/Nov 09:37

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa...

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

msumbanews.co.tz - 05/Nov 18:44

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWATAKA WADAU KUJIKITA VIJIJINI, ELIMU YA KUPINGA UKATILI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 08:24

  Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...

AICC NI MUHIMILI WA SEKTA YA UTALII NCHINI

msumbanews.co.tz - 01/Nov 09:36

 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan...

KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA KULETA UWEKEZAJI NA UBUNIFU MPYA TANZANIA -MHE. KADUARA

msumbanews.co.tz - 26/Oct 05:49

 Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Shaibu Kaduara amesema Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi Afrika...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément