Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 06 Novemba 2024 ameshiriki mazishi ya marehemu John Tutuba ambaye...
Vous n'êtes pas connecté
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Mizengo Pinda ameshiriki mazishi ya kuuanga Mwili wa marehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa ambaye alikuwa Jaji Msataafu wa Mahakama kuu ya Tanzania na aliyewahi kushika Nyadhifa mbalimbali Serikalini enzi za Uhai wake ikiwemo Katibu Wa Bunge.Hafla ya Mazishi yamefanyika leo Tarehe 06 November 2024 katika Kijiji cha Kinampanda Kilichopo katika wilaya ya Iramba Mkoani SingidaMhe. Pinda ameshiriki Mazishi hayo akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ameeleza kwa masikitiko juu ya kuondokewa na Marehemu. Jaji Kipenka Msemembo Mussa.Mazishi hayo yametanguliwa na Ibada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Wilayani Kinampanda na kuongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati, Dk. Cyprian HilintiAkitoa salamu za rambirambi, Naibu Waziri Pinda amesema kuwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Serikali nzima wanaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.Mhe. Pinda amesema marehemu Jaji Kipenka alikuwa kiungo muhimu cha Maendeleo kwa Wananchi wa Kinampanda enzi za uhai wake alikuwa akishirikiana vema na Dkt Mwigulu katika Shughuli mbalimbali za Maendeleo."Nimesimama hapa kwa niaba ya mhe. Mwigulu ambaye anatoa pole nyingi sana kwa familia na ameindokewa kwa maelezo yake na mtu muhimu ambaye kilikuwa Kiungo cha Maendeleo cha Kinampanda". Amesema Mhe PindaAidha Mhe. Pinda ametoa wito kwa familia ya Jaji Kipenka hasa watoto wa marehemu kuacha kugombania mali zilizokuwa zinamilikiwa na Marehemu Jaji Kipenka kwani Kifanya hivyo kutawaingiza matatizoni zaidi."Kikubwa kwenye familia mtulie wakati wa pito hilo katika kukusanya mali za marehemu", Amesema Mhe Pinda"Nimeona baba ana watoto wanne lakini watoto kokote waliko wasisahau Mwenza wa Marehemu Jaji Kipenka yupo hai". Amesema Mhe PindaMarehemu Jaji Kipenka Msemembo Mussa alizaliwa tarehe 28, Desemba 1954 ambapo aliugua kwa muda kabla ya kufariki tarehe 2 November 2024.Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 06 Novemba 2024 ameshiriki mazishi ya marehemu John Tutuba ambaye...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya...
Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na...
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemaliza mgogoro wa Ardhi wa Familia ya Bw. Emmanuel Corneli Mbunda na Mzee...
Na Gideon Gregory, Dodoma.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...
Na. Joseph Mahumi, WF, MorogoroSerikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiongoza Kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya Baraza la Mawaziri...
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameliomba Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na...
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo leo tarehe 31 Oktoba 2024 amemuwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Wakuu wa...